Rais Samiah wa Tanzania amekuwa anatoa kauli za kejeli . Ni kama ana dharau Sana. Kwa mfano aliwahi kutoa kauli ya kwamba katiba ni kijitabu tu. Kwa maana nyingine Katiba so Jambo la maana. Pia amewahi kunukuliwa akidai ya kwamba kifo ni kifo hakuna kifo kibaya zaidi ya kingine. Alisema maneno kama njia ya kuonesha ya kwamba kifo Cha kada wa CHADEMA Ally Kibao sio Jambo zito Sana.
Leo wakati akiapisha mawaziri , Rais amesikika akidai ya kwamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni Yusuf ameacha alama. Ni kipindi Cha Waziri Masauni kundi la watu kutekwa na kupotezwa limeshika kasi, mpaka kupelekea wananchi kujihami. Juzi tu hapa mfanyakazi wa TRA kauawa kisa hofu ya watu wasio julikana. Wananchi kutoamini vyombo vya Usalama ni ushahidi tosha ya kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani alipwaya.
Rais kuanza kumpa sifa za kinafiki ni kukejeli hali halisi ya Usalama nchini. Rais aache mashindano yupo pale kuwatumikia wananchi na Sio kuwakejeli. Ipo siku kejeli zake zitamtokea puani.