Rais Samia anawekeza sana kwenye kilimo lakini "strategy" Wizara ya Kilimo ni sifuri

Rais Samia anawekeza sana kwenye kilimo lakini "strategy" Wizara ya Kilimo ni sifuri

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Kiukweli wizara ya kilimo haina strategy yeyote inayoweza kukomboa kilimo chetu. Watu wengi unasikia kila mahali wakimsifu waziri bashe, ila ukiwauliza mnamsifu kwa lipi hasa alilolifanya? Hawana majibu.

Mimi namshauri Bashe afanye yafuatayo:
1.
Kwa soko la ndani Tanzania kwa sasa tunajitosheleza katika kilimo, mbinu zinazotumika ku "boost" uzalishaji wa ndani hazitaleta tija. Mnatumia majukwaa, mnatumia ruzuku kuhamasisha watanzania kuzalisha zaidi kwenye kilimo chao cha jadi walichokizoea, hii bila mpango madhubuti itaendelea kufanya kilimo kuonekana siyo fursa. mazao yataongezeka na hamuonekana kuwa na marketing strategy ya jinsi mazao yatakayoongezeka soko lake liko wapi? Mwisho wa siku itakuwa ni mazao kuongezeka lakini soko ni lilelile na kitakachotokea ni bei za mazao husika kuporomoka. hapo hamupromote kilimo bali mnakididimiza maana mnaweka mikakati ya kukatisha wakulima tamaa. Hakuna mkulima atakayeongeza uzalishaji mwaka unaofuata kama mazao ya msimu tunaoingia ama atauza kwa hasara au atakuwa nayo ndani yamekosa soko.

2. Ni lazima muwe na mkakati wa kutafuta masoko ya mazao nje ya nchi. Ni lazima wizara ya kilimo ifanye utafiti kujua masoko ya mazao ya kilimo nje yako wapi? mfano mnaweza kutafuta nchi za afrika zinazoagiza chakula nje kwa wingi ni zipi na zinaagiza nini na kwa bei gani? Tafuteni katika hilo soko Tanzania tunaweza kuingiaje. Mnaweza kutumia bei ya tani moja kufika nchi husika ikawa ya chini kulinganisha na wanavyonunua kwa sasa, mnaweza kutumia diplomasia kwa kuandaa ziara za mkuu wa nchi katika mataifa husika kutafuta masoko, ziara za waziri husika kutembelea nchi husika kutafuta masoko. Nchi haiwezi kukaa kuimba diplomasia ya uchumi alafu mkuu wa nchi anasafiri nje hatusikii hata kasaini mkataba wowote wa kuuza nje chakula.

3. mfumo wa ruzuku wa mbolea siyo ruzuku tunayoitaka kwa sasa hapa tulipo. mfumo huo ulifaa kwa kipindi ambacho nchi yetu ilikuwa haijitoshelezi kwa chakula. Malengo ya mfumo huo ulikuwa kuongeza uzalishaji kwa wakulima wa kilimo cha jadi kilichokuwa kikifanyika ili tanzania iache kuagiza nje chakula. Kwa sasa tulipofikia hatuhitaji ku boost kilimo kwa kuongeza productivity katika uzalishaji wa jadi, bali tunahitaji kuongeza uzalishaji kutoka katika mashamba makubwa. Hapa sina maana kwa mba nasapoti ule mpango wenu wa kutenga ardhi ya mashamba makubwa. Mipango kama hiyo mliyo nayo haitaendeleza kilimo chenu, mashamba yanaweza kuishia mikononi mwa wajanja wasiopenda kulima ila kuchukua mashamba kama asset. Mimi ninachokitamani ni mlete mpango wa watanzania wenyewe kuanza kulima mashamba makubwa, watoke kwenye kilimo cha jadi mtu awaze kulima ekari kadhaa. ili haya yatokee ni ninyi ku guantee soko la mazao. mfano mkitangaza kununua tani milioni 4 za mahindi msimu unaokuja na mkawatangazia kila mkoa ujue kwao mnanunua kiasi gani. viongozi wa serikali ngazi ya mkoa waanze kuhamasisha vijana kujiajiri katika kilimo. msimu ukiisha mnatazama kama wakulima wamelima zaidi mnaweza hata kuwakopa na kuingiza kwenye maghala alafu mnatafuta masoko nje.

Kilimo chetu bado hakitumii technolojia hivyo ili tuuze nje inabidi muweke ruzuku ili mkulima apate bei nzuri. mnaweza ku export kwa kila kilo moja ya mahindi shilingi 350 lakini nyinyi mnanunua kilo 500 (150 itakuwa ruzuku ya serikali)

Mkikibeba kilimo ndani ya miaka michache watanzania watakuwa na masoko yenye kuwezesha wakulima kununua mashine ya kisasa wenyewe na kuwekeza kwenye mifumo ya umwagiliaji na huko watazalisha kwa gharama kidogo na kuweza kutosheleza soko bila ruzuku. hivyo tazameni jinsi ruzuku kwenye export inavyoweza kuleta masoko.

4. Kuna kilimo kama cha vanira, ukienda kagera wakulima hawalimi mazao haya kwa kuogopa wizi. mtu akilima lazima ajiandae kulala shambani. wizara mnafanya nini kuja na mbinu za kuhamasisha hiki kilimo kwa kuondoa vitisho vya wizi na kuwaingiza wakulima kuzalisha mazao haya yenye soko kubwa nje kwa wingi.
 
Back
Top Bottom