Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

Rais wangu Samia Suluhu Hassan anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T | SG kwa TZS 6.5T na miradi mingine huku akiachilia vicheko kwa makundi mbalimbali ya watanzania,

" Hakuna kama Samia "


Ukichukua gharama za miradi miwili mikubwa ya SGR na SG|JNHPP inayoendelea kwa sasa yaani SGR Isaka -Mwanza kilometa 341 kwa TZS 3.02trl ,Makutupora-Morogoro kilometa 422 kwa TZS 4.4trl ,Dar -Morogoro kilometa 300 kwa TZS 2.7trl na SG|JNHPP $2.9BL au TZS 6.55trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine mipya na ile iliyoachwa na Hayati Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli miradi hii yote Rais Samia Suluhu Hassan anaziendeleza tena kwa BOQ zilezile,
===
Kutoka kwa Rais Samia kinachonivutia zaidi ni hivi vicheko kwa haya makundi mbalimbali najiuliza amewezaje yote haya yaliyowashinda watangulizi wake tena waliojiita wanaume wa shoka?!
===
Kicheko cha Rais Samia na wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 11 hawakupewa mikopo,Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020|21 hadi 570BL FY2021|22 na kufanya kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea,

===
Rais Samia amefuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika hao watakatwa 9% tu ( single digits) FY2021|22 kutoka 15% ya FY2020|21,Kwa lugha rahisi take home za watu hawa zimepaa kwa 6% nivicheko kila kona ya nchi na Rais Samia Suluhu Hassan,
===
Kicheko cha Rais Samia na Wafanyakazi,Sote tunafahamu,kwa miaka mitano ( 5 ) mfululizo tumeshuhudia wafanyakazi wa Umma hawajapandishwa vyeo|madaraja,lakini ndani ya miezi hii michache mama ameshatoa TZS 509BL, kwenye bajeti ya FY2021|22 Yaani 449BL za madaraja|vyeo na 60BL za malimbikizo ya mishahara na tayari Pesa hizi zimeleta vicheko kwa wafanyakazi,
===
Rais Samia amepunguza kodi (PAYE) toka 9% FY2020|21 mpaka 8% hivi sasa,Kwa utendaji huu hivi Wafanyakazi mnamtaka nani zaidi kama sio Rais Samia? kwa lugha rahisi FY2021|22 ameongeza mishahara ya wafanyakazi wote wa Serikali na binafsi kwa 1% kwa kuwarudishia hiyo 1% ya mishahara yao, na kwakufanya hivyo Serikali itatumia|itapoteza kiasi cha Tshs 14.1781BL kwenye bajeti yake ya FY2021|22 fedha ambayo itarudishwa kwa wafanyakazi kama nyongeza ya mishahara yao
===
Kicheko cha Rais Samia na wasio Ajiriwa,kwa mara ya mwisho ilikuwa FY2015|16 wakati wa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipoachilia ajira mpya elfu 52 trh 01|05|2015,Leo ni miaka mitano imepita ila kwa miezi michache ya Mama Samia tunashuhudia tena ajira mpya za Serikali elfu 40 kwa FY2021|22 kwa gharama ya Tshs 239BL na 120BL kwaajili ya kubadili muundo wa Utumishi,

===
Maajabu zaidi ya Mama Samia tayari amesajili miradi mikubwa mipya 93 yenye thamani ya $1.6BL karibu TZS 3.23trl ambayo nayo itaajiri watu 23,600 na kufanya ndani ya hivi vimiezi vichache Rais Samia atatoa Jumla ya nafasi 53,600 za ajira achilia mbali miradi mingine mingi ya sekta binafsi|Umma inayoendelea kutoa ajira lengo likiwa ni kufikia ajira 8M ifikapo mwaka 2025 kama Ilani inavyotaka,
===
Kicheko cha Rais Samia Majimboni,Bila kujali ukubwa wa jimbo Rais Samia FY2021|22 ameshatoa TZS 132BL sawa na Tshs 500M katika kila Jimbo kwa majimbo yote 264 kama fedha za maendeleo ya Jimbo hizi ni mbali na fedha za mfuko wa Jimbo,fedha hizi zimerudisha tabasamu kwa Wabunge hasa wa Majimbo,

===
Mama Samia ametoa tena TZS 322.158BL kama bajeti ya nyongeza kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba 10,000 vya madarasa Zahanati 555,Vituo vya afya 121,
===
Rais Samia hakuishia hapo bajeti ya TARURA pia ameiongeza kwa 254% yaani kutoka 273BL FY 2020|21 hadi 966.43BL FY2021|22 ili kumaliza kila barabara korofi Mjini na Vijijini|,Nimwendo wa vicheko tu Watanzania tumtake nani kama sio Samia?
===
Kicheko cha Rais Samia na wafanyabiashara|Wawekezaji, Mhe Rais Samia Ndio rais pekee aliyetangaza hadharani kuwa hahitaji kodi za Kishetani na akafuta jumla ya kodi|tozo zote kandamizi zipatazo 232 FY2021|22 bila kujali hasara ya Tshs 55.49997BL ambayo Serikali yake itapata kwa kuondoa tozo|kodi hizo nia yake aongeze idadi ya walipa kodi kutoka 3.4M waliopo na matokeo tayari wote tumeanza tumeyaona .

===
Nchi hii tangu tupate uhuru sijawahi kusikia tozo|kodi zaidi ya 230 zikifutwa kwa kwamkupuo Kama ambavyo mama ameachilia kicheko hiki kwani hataki kabisa Tax economy hakika kesho yetu ni bora sana,
===
Pamoja na kukataa kodi za kishetani na kuondoa tozo kandamizi bado Miradi yote ya Watangulizi wake anaiendeleza sawasawa ikiwemo SGR $4.64BL au TZS 10.2trl,SG $2.9BL au TZS 6.5trl,Ununuzi wa ndege mpya,barabara zote ujenzi unaendelea, madaraja yote,meli zote,
===
Pamoja na haya yote kufanyika bado Wafanyakazi wetu ni vicheko,Wafanyabiashara|wawekezaji wetu ni vicheko,bodaboda wetu ni vicheko, machinga wetu ni vicheko,wanafunzi wetu hasa wa elimu ya juu ni vicheko, wafugaji wetu ni vicheko,wakulima wetu ni vicheko, Wapinzani nao ni vicheko hata wewe unayesoma naamini, Tayari na wewe unakicheko chako umecheka na Mama Samia Suluhu
===
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
===


photo_2021-11-01_12-14-13.jpg
 
Wasalaam wanaJf,

Ukichukua gharama za miradi miwili tu mikubwa ya SGR na SG inayoendelea kwa sasa yaani Isaka -Mwanza 341km Tshs 3.02trl, Makutupora-Morogoro 422Km Tshs 4.4trl ,Morogoro -DSM 300Km Tshs 2.7trl na SG US$ 2.9BL Tshs 6.5trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine
Hatuna waziri wa ulinzi mpaka Sasa, haya komaa bwashee
 
Wasalaam wanaJf,

Ukichukua gharama za miradi miwili tu mikubwa ya SGR na SG inayoendelea kwa sasa yaani Isaka -Mwanza 341km Tshs 3.02trl, Makutupora-Morogoro 422Km Tshs 4.4trl ,Morogoro -DSM 300Km Tshs 2.7trl na SG US$ 2.9BL Tshs 6.5trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine
Shida ni kwamba amepoteza direction, Hana Legacy kama Rais. Hajulikani ni Maushungi au Meko anayejitahd kujinasibu nae-Angefanikiwa sana kama angetengeneza legacy yake alone.
 
Huyu mama aishi milele,

Mke wangu kalamba 250,000 daraja jipya,

Ndio kwa mara ya kwanza Sal Slip imebadilika tangu 2015.

Mimi na familia yangu tunamtaka huyuhuyu 2025,

Mbona anafanya yote yaliyofanywa na Magufuli na bado anaachia pesa, hayati alikwama wapi?
 
Gesi ya kupikia majumbani imepanda bei.

Mafuta ya kula yamepanda bei.

Tozo za miamala ziko juu.

Kesho tunaanza kulipia majengo kwenye LUKU, hii maana yake ni kwamba ukinunua umeme utapata units pungufu ili pesa nyingine iende kwenye kodi ya jengo hata kama jengo hilo unaloishi siyo mali yako.

Vyakula vimepanda bei.

Kodi za nyumba zimepanda bei.

Ndugu hivi bado unadiriki kusema Watanzania tumejaa vicheko???????????

Mimi nakwambia sasa hivi Watz wanalia mara 7 zaidi ya ilivyokuwa kipindi cha Mwendazake. Huyu Madam SSH nchi itamshinda kabla hata ya 2025.
 
Wasalaam wanaJf,

Ukichukua gharama za miradi miwili tu mikubwa ya SGR na SG inayoendelea kwa sasa yaani Isaka -Mwanza 341km Tshs 3.02trl, Makutupora-Morogoro 422Km Tshs 4.4trl ,Morogoro -DSM 300Km Tshs 2.7trl na SG US$ 2.9BL Tshs 6.5trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine yote ikiwemo mipya na ile iliyoachwa na Rais Magufuli yote mama anaziendeleza tena kwa BOQ zilezile,
Mpumbavu kwenye ubora wako,nawe anza kurembua kma yeye utapewa udc...huyo anachoweza ni kurembua
 
Mama ameshindwa kabla hajaanza.

Of course watu wa pwani hawajawahi kua viongozi wa maana.

Ni watu legelege, wamezoea maisha ya kitumwa, waarabu wamewatumikisha miaka na miaka.

Hii nchi kuendelea bado ina safari ndefu sana.


Kama ni kweli haya yote amefanya mbona kama anapatia sana, Huku mtaani sisi walau tumeanza kula vyombo mzee, Bia ilikuwa imekuwa anasa, ilikuwa ni Balimi, Balimi tu,

Ungetuambia amekosea au amepotosha wapi,
 
Wasalaam wanaJf,

Ukichukua gharama za miradi miwili tu mikubwa ya SGR na SG inayoendelea kwa sasa yaani Isaka -Mwanza 341km Tshs 3.02trl, Makutupora-Morogoro 422Km Tshs 4.4trl ,Morogoro -DSM 300Km Tshs 2.7trl na SG US$ 2.9BL Tshs 6.5trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine yote ikiwemo mipya na ile iliyoachwa na Rais Magufuli yote mama anaziendeleza tena kwa BOQ zilezile,

Kinachonivutia zaidi ni hivi vicheko kwa haya makundi mbalimbali najiuliza Rais Samia amewezaje yote haya yaliyowashinda watangulizi wake wote? Mfano:,


1. Kicheko cha Rais Samia na wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 10 hawakupewa mikopo,Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020/21 hadi 570BL FY2021/22 na kufanya kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea huku akifuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika watakatwa 9% ( single digits) FY2021/22 kutoka 15% ya FY2020/21,Kwa lugha rahisi take home za watu hawa zimepaa kwa 6% nivicheko kila kona ya nchi,
__________________________________

2. Kicheko cha Rais Samia na Wafanyakazi,Sote tunafahamu,kwa miaka mitano ( 5 ) mfululizo tumeshuhudia wafanyakazi wa Umma hawakupandishwa vyeo|madaraja,lakini ndani ya miezi hii michache mama ameshatoa Tshs 509BL,Yaani 449BL za madaraja|vyeo na 60BL za malimbikizo ya mishahara na tayari Pesa hizi zimeleta vicheko kwa wafanyakazi huku akipunguza kodi (PAYE) toka 9% FY2020/21 mpaka 8% hivi sasa,kwa lugha rahisi FY2021/22 ameongeza mishahara ya wafanyakazi wote wa Serikali na binafsi kwa 1% kwa kuwarudishia hiyo 1% ya mishahara yao, na kwakufanya hivyo serikali itatumia|itapoteza kiasi cha Tshs 14.1781BL fedha ambayo itarudishwa kwa wafanyakazi kama nyongeza,
__________________________________

3. Kicheko cha Rais Samia na wasio Ajiriwa,mwisho ilikuwa FY2015/16 wakati wa Mzee JK alipoachilia ajira mpya elfu 52 trh 01|05|2015,Leo miaka mitano baadae na nimiezi michache ya Mama Samia tunashuhudia tena ajira mpya za serikali elfu 40 kwa gharama ya Tshs 239BL na 120BL kwaajili ya kubadili muundo wa Utumishi,maajabu zaidi ya mama tayari amesajili miradi mikubwa mipya 93 yenye thamani ya US$ 1.6BL karibu Tshs 3.23trl ambayo nayo itaajiri watu 23,600 na kumfanya ndani ya hivi vimiezi vichache kutoa jumla ya nafasi 53,600 za ajira achilia mbali miradi mingine mingi ya sekta binafsi|Umma inayoendelea kutoa ajira lengo likiwa ni ajira 8M mwaka 2025.
__________________________________

4. Kicheko cha Rais Samia Majimboni,Bila kujali ukubwa wa jimbo ameshatoa Tsh 132BL sawa na Tshs 500M kila Jimbo kwa majimbo yote 264 kama fedha za maendeleo ya Jimbo mbali na fedha za mfuko wa Jimbo,fedha hizi zimerudisha tabasamu kwa Wabunge hasa wa Majimbo,Mama ametoa tena Tshs 322.158BL kama bajeti ya nyongeza kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba 10,000 vya madarasa Zahanati 555,Vituo vya afya 121,hakuishia hapo TARURA nao bajeti yao ameiongeza kwa 254% yaani kutoka 273BL FY 2020/21 hadi 966.43BL FY2021/22 kumaliza kila barabara korofi Vijijini|Mitaani,Nimwendo wa vicheko Tu,
__________________________________

5. Kicheko cha Rais Samia na wafanyabiashara|Wawekezaji, Mhe Samia Ndio rais pekee aliyetangaza hadharani hahitaji kodi za Kishetani na akafuta jumla ya kodi|tozo zote kandamizi zipatazo 232 bila kujali hasara ya Tshs 55.49997BL ambayo serikali yake itapata kwa kuondoa tozo|kodi hizo nia yake aongeze idadi ya walipa kodi kutoka 2.7M waliopo na matokeo najua wote tumeyaona ,Nchi hii tangu tupate uhuru sijawahi kusikia tozo|kodi zaidi ya 230 zikifutwa kwa kwamkupuo Kama ambazo mama ameachilia kicheko hiki kwani hataki kabisa Tax economy ,pamoja na kukataa kodi za kishetani na kuondoa tozo kandamizi bado Miradi yote ya Watangulizi wake anaiendeleza sawasawa ikiwemo SGR US$ 4.64BL au Tsh 10.2trl,SG US$ 2.9BL au Tshs 6.5trl,ndege Mpya,barabara zote ujenzi unaendelea, madaraja yote,meli zote pamoja na haya yote kufanyika bado Wafanyakazi wetu ni vicheko,Wafanyabiashara|wawekezaji wetu ni vicheko,bodaboda wetu ni vicheko, machinga wetu ni vicheko,wanafunzi wetu hasa wa elimu ya juu ni vicheko, wafugaji wetu ni vicheko,wakulima wetu ni vicheko, Wapinzani nao ni vicheko hata wewe unayesoma naamini, Tayari nawewe unakicheko chako umecheka na Mama Samia ,


" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"


Napenda sana akili za kiwango hicki, Napenda sana mtu anayeleta hoja zake kwa namba, Namba haijawi kusema uongo kamwe, Samia anavunja rekodi shida kubwa Team mwendazake inamvuta sana shati,

Kunywa soda mwandishi utalipa mwenyewe.
 
Huyu jamaa ni mzalendo sana, kila anacholeta hapa kinamaslahi kwa Taifa hata kama tunampinga,Mama Samia ni bonge la kiongozi ukiacha mapungufu machache ya kibinadamu,
Acheni basi jamaeni! kwani hamuwezi kaa kimya kama hakuna cha kuandika?

Hivi unajua biashara zimesimsma, watu wanakaa tu madukani hawauzi?
 
Punguza kujipendekeza mmeanza kujitokeza akina Musiba wa awamu hii.

Tumpe muda maana miradi yote iyo hakuna uliokamilika, asilimia moja yq kodi watumishi wamekutana na 2500 kama myongeza nadhani amewapa ya voc

Hiyo miaka 5 kwani aliipata hiyo pesa, Mwacheni mama wa watu achape kazi ila kama haya ni ya kweli basi kasi yake inatisha sana, kila hatua Dua
 
Napenda sana akili za kiwango hichi,Napenda sana mtu anayeleta hoja zake kwa namba, Namba haijawi kusema uongo kamwe, Samia anavunja rekodi shida kubwa Team mwendazake inamvuta sana shati,

Kunywa soda mwandishi utalipa mwenyewe,
Tulieni basi jameni, Hivi unajua kwamba kwa sasa wananchi wanakula mlo mmoja Kwamba pesa haipo?

Bidhaa zipo ila pesa haipo?
 
Huyu mama aishi milele,

Mke wangu kalamba 250,000 daraja jipya,

Ndio kwa mara ya kwanza Sal Slip imebadilika tangu 2015.

Mimi na familia yangu tunamtaka huyuhuyu 2025,

Mbona anafanya yote yaliyofanywa na Magufuli na bado anaachia pesa hayati alikwama wapi?
Kwamba kila mwezi atakuwa na nyongeza ya hiyo amount?

Basi mkapokee chanjo zenu haraka muungeni mkono mama yenu maana anaupiga mwingi sana.
 
Back
Top Bottom