Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

 
kwa mwezi ni 1.9T
 
Rais anawezaje yote haya kama sio mpango wa Mungu?
 
Maajabu
 
Mama chapa kazi
 
Umeandika mambo mazuri na nayakubali, ila unapiga pambio sana hizi pambio huwalevya viongozi wazuri kisha huwaharibu , nyie waimba kwaya mtaendelea na kwaya zenu maana ni kipaji chenu lakini usisahau kuwa wakati huo idadi kubwa ya wananchi itakuwa inaumia.

Weka data ,weka na hongera yako mwishoni inatosha.
 
Kazi iendelee
 
Asante Sana mkuu wangu
 
Mama ameshindwa kabla hajaanza.

Of course watu wa pwani hawajawahi kua viongozi wa maana.

Ni watu legelege, wamezoea maisha ya kitumwa, waarabu wamewatumikisha miaka na miaka.

Hii nchi kuendelea bado ina safari ndefu sana.
Sijui haya unayotoa kupitia mdomo gani! Mpuuzi mkubwa wewe. Mtu yeyote anaye 'generalise' hana akili na mod angefanya kazi yake (au pia anakubaliana na mwehu huyu?).
Licha ya kuwa unayosema ni uwongo, kwani kumepita viongozi wazuri sana kutoka Pwani (Mwinyi ambaye aliikuta nchi hii ina dollar 170 tu benki kuu, ilivyoachwa na huyo 'Mbara' wako). Na sasa Samia (hata kama bado) naye pia aliikuta nchi hii muflis kabisa na huyo Mbara mwenzio. On the contarry, Wapwani siku zote wametilia maanani zaidi ustawi wa watu as opposed na ustawi wa vitu unaoshabikiwa na 'Wabara'.
 
Daah
 
Hayati alikuwa anabeba mambo mengi ndani ya nafsi yake. Kaishi na machungu ya kila aina. Huyu Mama anaenda kulala usiku akiwa hajambeba mtu nafsini mwake.
 
Hayati alikuwa anabeba mambo mengi ndani ya nafsi yake. Kaishi na machungu ya kila aina. Huyu Mama anaenda kulala usiku akiwa hajambeba mtu nafsini mwake.
Sikulaumu wewe, nalaumu siasa za Kisoshalisti (aka Ujamaa). Moja ya mambo mabaya ya siasa hizi ni kuwaduwaza watu wafikirie kuwa serikali ina wajibu wa moja kwa moja kuwanyonyesha, kuwalisha, kuwaozesha na hadi kuwazika! Siasa hizo zina shabaha ya kukupa hayo, zinapoweza, kwa kubadilishana na roho yako, uhuru wako wa kifikra, kiitikadi na hata kisiasa. Zinadai zitakulea usiwe na hofu (Ndiyo maana bado hadi sasa tuna 'Baba wa Taifa!).
Jukumu la serikali ni kukupa fursa ukitaka kusoma usome, ukitaka tiba kuwepo na hospitali, ukitaka kufanya biashara kuwepo na miundo mbinu....lakini siyo 'kukushika mkono' au kama usemavyo, 'kubeba mtu nafsini mwa kiongozi'. Amka! Ujamaa ulishindikana. Na hata alipoujaribu hayati Magufuli, yaelekea huko alikokuwa anaelekea, angeshindwa pia. Pengine ni mfumo mzuri, lakini hatutajua, maana wote walioujaribu walishindwa katikati!
 
Una hoja lakini ipo tofauti kabisa na lengo langu. Kumbeba mtu usiku namaanisha tabia ya ugomvi anayokuwa nayo mtu.

Tabia ya kufuatilia kila kitu hata yale masuala yanayoonekana ni madogo kwa fikra za haraka za kibinadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…