Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?

Hili andiko nimeli"save "Mahala huwa nalipitia taratibu,
 
Andiko




Andiko bora kabisa hili la zama za Rais Samia,
 



Rais Samia anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T na SG kwa TZS 6.55T?​

1 of 18Next Last
Jump to newIgnoreUnwatch
[IMG alt="CM 1774858"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/635/635023.jpg?1634462201[/IMG]

CM 1774858

JF-Expert Member​

Rais wangu Samia Suluhu Hassan anawezaje kujenga SGR kilometa 1,063 kwa TZS 10.1T | SG kwa TZS 6.5T na miradi mingine huku akiachilia vicheko kwa makundi mbalimbali ya watanzania,​

" Hakuna kama Samia "​

Ukichukua gharama za miradi miwili mikubwa ya SGR na SG|JNHPP inayoendelea kwa sasa yaani SGR Isaka -Mwanza kilometa 341 kwa TZS 3.02trl ,Makutupora-Morogoro kilometa 422 kwa TZS 4.4trl ,Dar -Morogoro kilometa 300 kwa TZS 2.7trl na SG|JNHPP $2.9BL au TZS 6.55trl Jumla yake ni Tshs 16.6trl achilia mbali miradi mingine mipya na ile iliyoachwa na Hayati Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli miradi hii yote Rais Samia Suluhu Hassan anaziendeleza tena kwa BOQ zilezile,
===
Kutoka kwa Rais Samia kinachonivutia zaidi ni hivi vicheko kwa haya makundi mbalimbali najiuliza amewezaje yote haya yaliyowashinda watangulizi wake tena waliojiita wanaume wa shoka?!
===
Kicheko cha Rais Samia na wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 11 hawakupewa mikopo,Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020|21 hadi 570BL FY2021|22 na kufanya kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea,
===
Rais Samia amefuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika hao watakatwa 9% tu ( single digits) FY2021|22 kutoka 15% ya FY2020|21,Kwa lugha rahisi take home za watu hawa zimepaa kwa 6% nivicheko kila kona ya nchi na Rais Samia Suluhu Hassan,
===
Kicheko cha Rais Samia na Wafanyakazi,Sote tunafahamu,kwa miaka mitano ( 5 ) mfululizo tumeshuhudia wafanyakazi wa Umma hawajapandishwa vyeo|madaraja,lakini ndani ya miezi hii michache mama ameshatoa TZS 509BL, kwenye bajeti ya FY2021|22 Yaani 449BL za madaraja|vyeo na 60BL za malimbikizo ya mishahara na tayari Pesa hizi zimeleta vicheko kwa wafanyakazi,
===
Rais Samia amepunguza kodi (PAYE) toka 9% FY2020|21 mpaka 8% hivi sasa,Kwa utendaji huu hivi Wafanyakazi mnamtaka nani zaidi kama sio Rais Samia? kwa lugha rahisi FY2021|22 ameongeza mishahara ya wafanyakazi wote wa Serikali na binafsi kwa 1% kwa kuwarudishia hiyo 1% ya mishahara yao, na kwakufanya hivyo Serikali itatumia|itapoteza kiasi cha Tshs 14.1781BL kwenye bajeti yake ya FY2021|22 fedha ambayo itarudishwa kwa wafanyakazi kama nyongeza ya mishahara yao
===
 
Kazi iendelee,
 
Inahitaji akili mingii sana kumuelewa SSH.
 
Hivi anayeongoza Serkali huajiri watu wa KUPIGA MAPAMBIO na KUSIFU, ? Nauliza tu. Maana kila zama na ngojera na wapiga zumali .

Afrika tutafika kweli, kama mtu au kikundi kimeajiri kusifu, bila kuhoji? Tangu kipindi
Zidumu FIKRA SAHIHI za Mwenyekiti hadi sasa
 
Nani kaajiriwa ili kusifu?
 
Huwa sina tabia ya kusifu kama sikosoi pia. Kwenye mambo mazuri nitasifu kwenye amekosea nitasema (kukosoa).

Suala la kesi ya Mbowe nilimpinga wazi wazi, alicheza branda.
 
Huwa sina tabia ya kusifu kama sikosoi pia. Kwenye mambo mazuri nitasifu kwenye amekosea nitasema (kukosoa).

Suala la kesi ya Mbowe nilimpinga wazi wazi, alicheza branda.
Rais wetu ni msikivu sana,
 
Shida ni kwamba amepoteza direction, Hana Legacy kama Rais. Hajulikani ni Maushungi au Meko anayejitahd kujinasibu nae-Angefanikiwa sana kama angetengeneza legacy yake alone.
Unamshauri hivi kwa hiyo aache ya Magu aanzishe zake kama Magu alivyofanya? Huko kutapoteza hela nyingi sana kwani matrilioni yameshatumika kwenye miradi hiyo. Sii busara kabisa kumshauri atafute legacy yake aachane na za Magu.
 
Unamshauri hivi kwa hiyo aache ya Magu aanzishe zake kama Magu alivyofanya? Huko kutapoteza hela nyingi sana kwani matrilioni yameshatumika kwenye miradi hiyo. Sii busara kabisa kumshauri atafute legacy yake aachane na za Magu.
Na ndicho kinafanyika ....Rostam anakuja na umeme wake baada ya ziara ya "Royal Tour" kulikuwa na mkataba wa trillions wata-share kwamba msimamizi wao kwenye vile vijiji na maeneo ambayo hayana umeme wa Tanesco. Bwawa la Nyerere kesi imeshafufuliwa kwamba ni uharibifu wa mazingira... even though kesi ya kwanza tulishinda kupitia Kabudi so bwawa lina pigwa chini soon utaniambia... ingawa watahangaika sana.
 
Unamshauri hivi kwa hiyo aache ya Magu aanzishe zake kama Magu alivyofanya? Huko kutapoteza hela nyingi sana kwani matrilioni yameshatumika kwenye miradi hiyo. Sii busara kabisa kumshauri atafute legacy yake aachane na za Magu.
Lini kasema anaachana na miradi ya Magu?
 
Nailed
 
Du ile miti waliouza hivi CAG aliipitia unaweza kuta waligawana na ndugu zake. Hata usipolimaliza walishaharibu mazingira vya kutosha. Sii busara kuliacha lilipofikia, ila tija yake haitafikia lilipokusudiwa kwa ajili ya adhari za kimazingira zinazofanyika kwenye catchment ya bonde hilo kuanzia Mbeya, Iringa, Lindi na Morogoro yenyewe. Ufugaji umetamalaki maeneo yote hayo na kufungua mashamba katikati ya misitu ya asili.
 
Tupigeni kazi sasa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…