Hamduni
Senior Member
- Apr 25, 2020
- 172
- 118
BAJETI YA SERIKALI 2022/2023 ILIVYOGUSA MAISHA YA VIJANA
(Rais Samia anaziishi ahadi zake kwa vitendo)
Na Victoria Charles Mwanziva. Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
Jambo kubwa lililokua linasubiriwa na vijana wengi wa Tanzania ni bajeti kuu ya serikali 2022/2023 ili kuona ni namna gani itakugusa maisha yao wakizingatia matokeo makubwa yaliyopatikana katika bajeti ya kwanza ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan 2021/2022 amabaye amefanya mambo makubwa na yanayoonekana hili liliwavuatia wengi kuisubiri kwa hamu bajeti ya 2022/2023 wakiamini mambo makubwa Zaidi yanakwenda kufanyika yanayowagusa moja kwa moja.
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ni aina ya kiongozi anayeziishi ahadi zake kwa vitendo, tumeshuhudia asilimia kubwa ya yaliyokua yameainishwa kwenye bajeti kuu ya 2021/2022 yakitekelezwa kwa ufanisi mkubwa na matokeo yake yapo wazi kila mtanzania anayashuhudia ni kwa namna gani yameweza kumgusa moja kwa moja katika maisha yake ya kila siku.
Kabla ya kuanza kuelezea kwa kiasi gani bajeti ya 2022/2023 Serikali ya Rais Samia Imedhamiria nini katika kuwaletea wananchi maendeleo napenda kuanza kuyataja mambo amabayo yaliahidiwa katika bajeti ya 2021/2022 na yameshatekelezwa kwa 100%.
Katika bajeti ya 2021/2022 Mhe Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo mengi sana ambayo moja kwa moja yanawagusa Vijana wa Tanzania baadhi ya aliyoyafanya ni. Amepunguza kodi ya mshahara (Paye) kutoka 9%-8%, ametengeneza Ajira rasmi 44,000, amefanya mabadiliko ya Muundo wa Utumishi, Kapandisha Vyeo Watumishi 190,562, Kalipa malimbikizo ya Mishahara, Kahakikisha ulipwaji Mafao ya Wastaafu kwa wakati, Kafuta tozo ya 6% Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu, Kaongeza Umri wa Utegemezi wa Mtoto Kutoka miaka 18-21, Kaboresha Mazingira ya Utendaji kazi kwa watumishi wa Umma, kapitisha marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Walimu, Kaongeza Mishahara kwa watumishi wa umma, kaendeleza miradi ya kimakakati kama SGR na Bwawa la kuzalisha umeme la mwalimu Nyerere, Ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule za Msingi na Sekondari, ujenzi wa nyumba za watumishi, ujenzi wa barabara, madaraja na vivuko, Ununuzi wa ndege mpya 5 na usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za umma jambo lililopelekea kuomgezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
Kwa kazi hio kubwa aliyoifanya Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwaka mmoja ni dhahiri sasa katika bajeti hii mpya mambo mengi makubwa yanaenda kufanyika ambayo yana tija kwa Taifa letu na manufaa makubwa kwa vijana. Maono ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona Tanzania inakua kimaendeleo na wananchi wake wanakua sehemu ya maendeleo hayo, katika hotuba zake maeneo mbalimbali ameweka bayana nia yake ya dhati ya kuwainua wananchi wa Tanzania kiuchumi.
Katika Bajeti ya mwaka huu yaani 2022/2023 Rais Samia ameendelea kudhihirisha ni kwa kiasi gani ana maona makubwa ya kuhakikisha matamanio ya watanzania walio wengi hususani vijana yanafikiwa kupitia utekelezaji wa miaradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mahususi za kimaendeleo ikiwemo kilimo, uwekezaji, Biashara, Ufugaji, Madini, Ujenzi na Uchukuzi.
Tumeshuhudia bajeti ya kipekee sana ikisomwa Bungeni na Waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, bajeti ambayo kwangu mimi naweza kuiita bajeti ya wananchi kwani inagusa kila eneo muhimu la maisha ya watanzania wote, bajeti ambayo haijamuacha hata mtu mmoja nyuma. Watanzania wameona mabilioni ya fedha yakitengwa na kuongezwa kwenye sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi na kuleta tija kwaTaifa letu.
Mhe Rais Samia Suuhu Hassan ametenga kiasi cha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vya VETA nchi nzima kwenye wilaya ambazo hazina vyuo hivyo lakini pia ameongeza bajeti ya kilimo kutoka bilioni 294 2021/2022 hadi kufikia shililing bilioni 954 bwjeti 2022/2023, ameongeza bajeti ya Uvuvi kutoka bilioni 168.25 2021/2022 hadi kufikia bilioni 268.25. Kuongezwa kwa bajeti katika sekta hizi muhimu za uzalishaji rasilimali watu, malighafi za viwandani na Chakula zinakwenda kuboresha uzalishaji katika maeneo hayo vile vile kuzalisha ajira kwa wingi kwa kundi adhimu la vijana wa Tanzania.
Mbali na uboreshwaji wa bajeti katika maeneo hayo muhimu ambayo ni dira ya ajira za vijana wengi wa Tanzania. Pia Mhe Samia Suluhu Hassan amefuta ada kwa wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita hivyo kufanya elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi kidato cha sita kwa shule za serikali, huku serikali ikiangalia namna ya kusaidia upatikanaji wa ujuzi na elimu kwa vyuo vya kati katika mfumo huo. Sanjari na hayo Mhe Samia ameondoa VAT kwenye maeneo kadhaa muhimu ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi wake. Baadi ya VAT alizozifuta ni , kwenye Miti amabyo haijachakatwa, Uzalishaji wa Mitungi ya gesi, Mafuta ya kula yanayozalishwa nchini, kwenye Maziwa mtindi pamoja na vifungashio vya maziwa, na kwenye simu janja.
Mhe Rais Samia hajawasahau wamachinga ambao asilimia kubwa ni Vijana na katika bajeti yake serikali imejipanga kuanza kutoa mikopo kwa wamachinga, hii ni hatua nzuri na nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa wamachinga wanaweza kukuza mitaji yao na kujiendelea kimaisha kupitia biashara zao ndogo ndogo wanazozifanya na kuchangia katika maendeleo ya Taifa. Lakini kuadhimia kupunguza kwa tozo za miamla ya simu kutokuzidi shilingi 4,000 kwa muamala ni ishara njema na unafuu mkubwa wa vijana wengi ambao wamejiajiri kwenye eneo hili.
Rai yangu kwa Vijana wenzangu, nawasihi sana vijana tumuunge mkono Mhe. Rais saia Suluhu Hassana katika shughuli mbalimbali za maendeleo anazozifanya kwa Taifa letu, tuwe wazalendeo kwa kuyasema mema mengi anayoyafanya Mama yetu Samia na tufanye kazi kwa bidii kwa maslahi yetu pamoja na Taifa letu kwa Ujumla.
Viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maslahi ya Vijana katika Wizara, Bungeni, na katikamashirikayote ya umma wahakikishe wanatimiza adhima ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo juu ya Vijana. Bajeti tumeiona, tumeielewa na maeneo yanayowhusu Vijana tumeyaoana na tumemuelewa sana Mhe Rais dhamira yake kwavijana hivyo hatutokaa kimya wala kufumbia macho pale ambapo tutaoana dhamira ya Mhe. Rais kwa Vijana inakwamwishwa mahali popote pale.