Jacob Mulikuza
Member
- Jul 15, 2021
- 16
- 61
Katika hotuba mbalimbali za Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha nia yake ya dhati kukuza uchumi wa taifa letu pamoja na kustawisha ustawi wa mtu na maendeleo yake. Haya ameyasisitiza katika hotuba zake wakati wa siku ya wafanyakazi na alipokutana na wazee wa Dar es Salaam. Katika hafla hizi mbili, amesisitiza dhamira yake ya kuboresha maslahi ya watumishi kwa kuongeza mishahara, kuboresha maisha ya wazee, kuboresha makazi ya wazee, kusisitiza haja ya matunzo kwa wazee kupitia jamii zetu na kufanya maboresho ya sheria zinazoonekana kukandamiza utu na ustawi wake.
Dhamira ya Rais Samia ni ya kweli na inahitaji kuungwa mkono kwa jitihada za pamoja zitakazoleta matunda ya haraka. Kwa maoni yangu kilimo ambacho kimeajiri takribani asilimia 75 ya watanzania ndio sehemu kubwa ya ushiriki wetu kama wananchi tunaweza kuchochea ukuaji wa uchumi kwa haraka sana.
Sekta zingine za uchumi ni za muhimu sana ila kilimo ndio sekta pekee ambayo tukiamua kufunga mkanda kwa muda wa miaka michache itatusaidia kukuza uchumi haraka sana na kusaidia sekta zingine za uchumu kukua kwa kasi sana. Mchango wa kilimo kwenye uchumi wetu ni taktribani asilimia 19.4 kwa mujibu wa takwimu za NBS za mwaka 2020. Sekta ya kilimo ni ya pili baada ya sekta ya ujenzi iliyochangia uchumi kwa asilimia 25.6 na ya tatu ikiwa sekta ya viwanda asilimia 9.8 na ya nne ikiwa mawasiliano na uchukuzi asilimia 8.8.
Kutokana na mabadiliko ya teknolojia na mawasiliano kilimo kimepoteza mvuto kwa watanzania wengi na kukifanya kuwa nafasi ya pili kwenye mchango wa pato la taifa ili hali kilimo kinamchango mkubwa kwenye pato la taifa kama taifa litaweka mkazo na kurejesha kilimo kuwa chenye tija na mvuto kwa watanzania ambao wameshakata tamaa ya kilimo cha jembe la mkono. Ukifuatilia takwimu za NBS mwaka 2000 utaona kilimo kilikuwa na mchango mkubwa kwenye pato la taifa kuanzia mwaka 1967 (asilimia 25.2), 1995 (asilimia 62.3) mpaka 2005 (asimilia 34.2) ndipo sekta ya kilimo ilipoanza kuwa ya pili kwenye mchango wa taifa mwaka 2015 (asilimia 12.7).
Kilimo kimejulikana kama uti wa mgongo wa taifa ila kwa mabadiliko ya sasa kilimo ni Oksijeni ya taifa kwani bila kilimo hakuna maendeleo endelevu. Vijana wengi wamejitenga na kilimo kwani kimepoteza mvuto na kuwafanya vijana wengi kuamini kilimo ni umasikini kutokana wakulima wengi wadogo kuwa kwenye dimbwi kubwa la umasikini hivyo kuwakatisha tamaa vijana wengi na kuchukia kilimo. Kutokana na kukosekana kwa mvuto wa kilimo, vijana wengi wamekimbilia mijini kwa matumaini ya kupata ajira rasmi ama kujiingiza kwenye ajira zisizo rasmi kwa nia ya kupata kipato ambapo mchango wake kwa taifa umekuwa mdogo sana. Takwimu za Umoja wa Mataifa za mwaka 2020 zinaonyesha kuwa vijana wa umri wa kati ya miaka 15-35 wasio na ajira ni asilimia 3.6. Tatizo hili ni kubwa na vijana wengi wangeweza kumezwa na sekta ya kilimo na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kabisa Tanzania.
Rais Samia akianza kuweka kipaumbele kwenye sekta ya kilimo ni dhahiri atapunguza tatizo la ukosefu wa ajira, ataweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma, ataweza kulipa posho kwa wazee kwa mwezi, ataweza kuwekeza kwenye miradi ya mikakati mingi na mikubwa zaidi, atachochea ukuwaji wa viwanda vingi, atakuza sekta binafsi kwa wingi na kubwa zaidi ataboresha ustawi wa watu, afya njema na elimu.
Rais Samia aanze kubadili namna kilimo kinavyoendeshwa Tanzania, kwani kwa vile kilivyo hakivutii na kinakatisha tamaa watu kujihusisha kutokana na ukosefu wa masoko, bei elekezi na mitaji.
Ili kilimo kiwe na tija na mvuto lazima turejeshe kilimo kwenye mitaala ya elimu ili kukifanya kilimo kuwa Oksijeni ya taifa. Vijana lazima wakue wakikijua kilimo na kupata mbinu bora na za kisasa za kufanya kilimo. Hapo awali kilimo kilikuwa kwenye mtaala wa elimu kisha kikafutwa na hapo ndipo kilimo kilipoanza kupoteza dira. Pia, kulikuwa na shule za mchepuo wa ufundi na kilimo kama vile Ifunda, Tanga, Moshi, Mtwara, Iyunda, Musoma na nyingine nyingi. Zote hizi zimegeuzwa kuwa shule za sekondari za kawaida zikitoa elimu ya nadharia tu. Tuanze shuleni kurejesha kilimo vijana wajifunze kwa nadharia na vitendo kisha baada ya hapo wanaweza kujiajiri kwa uhakika zaidi.
Serikali inapaswa kuwa mdhamini wa wakulima wote nchini wadogo na wakubwa kwa kutafuta masoko ya uhakikia ndani na nje ya nchi ili wakulima wapate soko la uhakika. Soko huria kwa asilimia kubwa limechangia kuzorotesha sekta ya kilimo kwani wakulima wakubwa tu ndio wamekuwa na uwezo wa kupata masoko kwa bei shindani lakini asilimia kubwa ya wakulima wadogo wameshindwa kupata masoko ya uhakika na kuishia kuzulumiwa na madalali. Serikali kazi yake kubwa itafute masoko ya uhakika yatakayopatikana kwa wakulima wadogo na wakubwa.
Kuwepo na vyama vya ushirika vinavyotokana na wakulima wenyewe badala ya vile ilivyo sasa ambapo wakulima wemekuwa huria na wanakosa chombo cha kuwasimamia na kujiendesha. Sambamba na hili upatikanaji wa pembejeo za kilimo utakuwa mrahisi kama vyama vya ushirika vitakuwa imara na kupata msaada wa serikali. Uwepo wa vyama vya ushirika imara utarahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, masoko ya uhakika, pembejeo za kilimo, ushauri wa kitaalamu na mengine mengi. Ni busara sasa Wizara ya kilimo kufanya utafiti wa kina kuona mchango wa vyama vya ushirika vikongwe kama KNCU viliwezaje kuwa vyama imara zaidi Afrika miaka ya nyuma na kuboresha mfumo huo utakorejesha kilimo kwa wananchi na kuleta manufaa kwa nchi.
Skimu za umwagiliaji maji nazo ni muhimu sana kujengwa na kuboreshwa na serikali kwani zitachangia ukuwaji wa sekta ya kilimo kwani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi mvua zimekuwa za kusuasua sana. Uzuri wa nchi yetu ikipata mvua inakuwa na maji ya kutosha ila mara nyingi mvua hizi zinaleta madhara na tunashindwa kuhifadhi maji haya ili yatumike pindi mvua zikikata. Vijana wabunifu wengi wapo wenye uwezo kwa kutengeneza skimu za kisasa za kutunza maji ni muda muafaka sasa watumike.
Natambua fika serikali inamikakati mingi kwenye kilimo, ila, ni muhimu sasa mikakati hiyo na mingine mingi ikawa shirikishi kwa wakulima ili kupata muafaka wa pamoja kuboresha kilimo chetu. Kilimo kikiboreshwa uchumi wa nchi utakuwa kwa haraka sana na kwa muda mfupi kuliko kutegemea sekta zingine za uchumi. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa nchi ya China ilianza kupata maendeleo makubwa kuanzia mwaka 1949 kwa kupita kilimo ambacho kimechangia ukuwaji wa sekta zingine kama tunavyoshughudia leo hii.
Rais Samia Suluhu anza kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwa nguvu zote kwa miaka mitano tu, utapata maendeleo ya hali ya juu kwa taifa na kwa watu wako. Msisitizo wa kutumia kilimo ni kwasababu ni sekta shirikishi ambayo watu tukifunga mkanda kwa miaka michache tutakuwa kikapu cha chakula Afrika na duniani na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 100.

Upvote
10