Rais Samia aongoza Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, leo Aprili 26, 2024

Rais Samia aongoza Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, leo Aprili 26, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, leo Aprili 26, 2024 ambapo Marais na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamehudhuria.



20240426_130851.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.

20240426_132439.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa katika Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.

20240426_132722.jpg
Rais akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


 
Ni maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia awaongoza Marais wa Africa kwenye tukio hili muhimu Sana

Sherehe ziko mubashara TBC

Jumaa Mubarak 😄
 
All is nothing if peoples lives are not improved by muungano
 
Ni maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia awaongoza Marais wa Africa kwenye tukio hili muhimu Sana

Sherehe ziko mubashara TBC

Jumaa Mubarak 😄
haisaidii loote kama ndani kuna wauaji, watekaji, wapoteza watu etc etc
Tunataka katiba mpya siyo marais kuja hapa
 
MUUNGANO NI TUNDA TAMU LA MTI WA UPENDO ( AMANI KARUME -ASP NA MWL JULIUS NYERERE - TANU )

Miaka 60 ya Muungano.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza Dr Samia Suluhu Hasan na Dr Husein Mwinyi kwa kutupa uhuru na amani katika kusheherekea siku ya Muungano ikiwa ni miaka 60 sasa tangu Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuwa kitu kimoja Tanzania ( Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania )

Zipo sababu za msingi sana za kuunganisha nchi hizi mbili kiuchumi, kiusalama na kijamii, maono ya mbali ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Mwalimu Julias Nyerere leo yanatufanya kujimwayamwaya katika nchi yetu yenye amani na utulivu, huku suala la usalama wa nchi likiwa ni la kiwango cha kipekee, wana siasa tunazichapa siasa kweli kweli.

PONGEZI KUBWA KWA MAMA KIZI MKAZI, DR SAMIA SULUHU HASANI

NDIMI
Comrade Ally Maftah
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Mjumbe Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
JITU LA MIRABA
CHALINENEE
KATIBA MPYA, TUME HURU, KIKOKOTOO, SHERIA NZURI, JESHI LA POLISI LA UADILIFU. HAYA YA SHEREHE HAYATUSAIDII LOLOTE, WASTAGE OF TIME
 
Mkuu Mohamed Said popote ulipo hapa JF naomba unipe history ya hiki Kikosi cha Tarabushi

Tarabushi Leo ndio wamekuwa Nyota ya sikukuu ya Miaka 60 ya Muungano

Ahsanteni Sana 😂😂
 
VIONGOZI WA UWT WASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Chatanda (MCC) akiwa na Viongozi wa UWT Taifa wameshiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Aprili 26, 2024.

#UWTImara
#JeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee

IMG-20240426-WA0064.jpg
IMG-20240426-WA0061.jpg
IMG-20240426-WA0066.jpg
IMG-20240426-WA0065.jpg
IMG-20240426-WA0058.jpg
IMG-20240426-WA0057.jpg
 
VIONGOZI WA UWT WASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Chatanda (MCC) akiwa na Viongozi wa UWT Taifa wameshiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Aprili 26, 2024.

#UWTImara
#JeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee
well done WUT comrades 💪👊
 
Jana kulifanyika Sherehe kubwa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa kweli Sherehe hii ilifana sana japo kulikuwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha. Hongera sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar.
 
Back
Top Bottom