Rais Samia aongoza Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, leo Aprili 26, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, leo Aprili 26, 2024 ambapo Marais na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamehudhuria.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa katika Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.

Rais akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


 
Ni maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia awaongoza Marais wa Africa kwenye tukio hili muhimu Sana

Sherehe ziko mubashara TBC

Jumaa Mubarak πŸ˜„
 
All is nothing if peoples lives are not improved by muungano
 
Ni maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia awaongoza Marais wa Africa kwenye tukio hili muhimu Sana

Sherehe ziko mubashara TBC

Jumaa Mubarak πŸ˜„
haisaidii loote kama ndani kuna wauaji, watekaji, wapoteza watu etc etc
Tunataka katiba mpya siyo marais kuja hapa
 
KATIBA MPYA, TUME HURU, KIKOKOTOO, SHERIA NZURI, JESHI LA POLISI LA UADILIFU. HAYA YA SHEREHE HAYATUSAIDII LOLOTE, WASTAGE OF TIME
 
Mkuu Mohamed Said popote ulipo hapa JF naomba unipe history ya hiki Kikosi cha Tarabushi

Tarabushi Leo ndio wamekuwa Nyota ya sikukuu ya Miaka 60 ya Muungano

Ahsanteni Sana πŸ˜‚πŸ˜‚
 
VIONGOZI WA UWT WASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Chatanda (MCC) akiwa na Viongozi wa UWT Taifa wameshiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Aprili 26, 2024.

#UWTImara
#JeshiLaMamaSamia
#KaziIendelee

 
well done WUT comrades πŸ’ͺπŸ‘Š
 
Jana kulifanyika Sherehe kubwa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa kweli Sherehe hii ilifana sana japo kulikuwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha. Hongera sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…