Rais Samia aorodheshwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi Barani Afrika

Rais Samia aorodheshwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi Barani Afrika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (Mama wa vitendo) aorodheshwa na kutambulishwa Dunia kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.

Ripoti ya Avance Media (100Women | Avance Media | 100 Most Influential African Women) yenye Makao Makuu yake Accra, Ghana ambayo ni wakala wa vyombo vya habari inayofuatilia masuala mbalimbali katika jamii barani Afrika. Fursa hii ya kuwa mmoja ya wanawake wenye ushawishi itumike vema kutangaza filamu ya Royal Tour ambayo inalenga kuitangaza Tanzania kimataifa huku Mhe. Rais akiwa mshiriki Mkuu wa filamu hiyo.

#TwendePamoja #KwaMatokeoyaHaraka


 
Amemshawishi nani na nani?
Ama wanasema kinyume kinyume, yaani Samia ni miongoni mwa wanawake 100 maarufu hapa Afrika asiyekuwa na ushawishi wowote kwa watu.

Embu waza tu kuhusu chanjo ya Covid, toka mama achanje hadharani zaidi ya mwezi mmoja uliopita ili kushawishi umma wa watanzania nao ukachanje mpaka sasa watanzania waliokubali kuchanjwa ni chini ya 1%.
 
Mama amefanikiwa kuiweka nchi katika misingi na mazingira mazuri baada ya kuwadhibiti wahuni wachache waliotaka kuiharibu nchi kupitia mambo ya kijinga. Ametambua ule msemo unaosema "ukicheka na nyani shambani utaambulia mabua" .
 
Sisi waswahili lazima tutauliza, je kamshawishi nani 😁
 
Duuh kwa hiyo katika hiyo orodha anashika namba 100?
 
Je, ni Nani anagharamia huo utalii ??? aka Royali tuwa ? Au kuna mfadhili ? Je ghalama za igizo hilo bajeti yake na makisio ni shilingi ngapi ?
 
Royal Tour sio kwa ajili ya Rais wetu peke yake. Ni series ambayo inatembelea nchi kadhaa na kumtumia kiongozi wa nchi kuitambulisha kwa dunia. Hivi karibuni ilikuwa Ecuador ambako Rais wake alikuwa ndio guide.

Amandla...
 
ROYAL TOUR, Wamebuni mbinu ya kuzoa fedha ikulu. Mwiongoni mwa wanawake 100 Africa?Nikidhani ni wapili au watatu ukixingatia kuwa ni Rais.
 
Naomba cost benefit analysis report ya mradi huu. Msinitumie inbox report hiyo. Mniwekee hapa hapa. Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom