Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (Mama wa vitendo) aorodheshwa na kutambulishwa Dunia kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.
Ripoti ya Avance Media (100Women | Avance Media | 100 Most Influential African Women) yenye Makao Makuu yake Accra, Ghana ambayo ni wakala wa vyombo vya habari inayofuatilia masuala mbalimbali katika jamii barani Afrika. Fursa hii ya kuwa mmoja ya wanawake wenye ushawishi itumike vema kutangaza filamu ya Royal Tour ambayo inalenga kuitangaza Tanzania kimataifa huku Mhe. Rais akiwa mshiriki Mkuu wa filamu hiyo.
Amemshawishi nani na nani?
Ama wanasema kinyume kinyume, yaani Samia ni miongoni mwa wanawake 100 maarufu hapa Afrika asiyekuwa na ushawishi wowote kwa watu.
Embu waza tu kuhusu chanjo ya Covid, toka mama achanje hadharani zaidi ya mwezi mmoja uliopita ili kushawishi umma wa watanzania nao ukachanje mpaka sasa watanzania waliokubali kuchanjwa ni chini ya 1%.
Amemshawishi nani na nani?
Ama wanasema kinyume kinyume, yaani Samia ni miongoni mwa wanawake 100 maarufu hapa Afrika asiyekuwa na ushawishi wowote kwa watu...
Mama amefanikiwa kuiweka nchi katika misingi na mazingira mazuri baada ya kuwadhibiti wahuni wachache waliotaka kuiharibu nchi kupitia mambo ya kijinga. Ametambua ule msemo unaosema "ukicheka na nyani shambani utaambulia mabua" .
Royal Tour sio kwa ajili ya Rais wetu peke yake. Ni series ambayo inatembelea nchi kadhaa na kumtumia kiongozi wa nchi kuitambulisha kwa dunia. Hivi karibuni ilikuwa Ecuador ambako Rais wake alikuwa ndio guide.