Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Amepokea Tuzo ya Gates Goalkeeper Awards Hyatt Regency Hotel Dar es salaam, leo tarehe 04 Februari, 2025.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo ametoa hutoba ambapo Rais Samia ameeleza kuwa idadi ya wataalamu wa afya hususani wa afya ya uzazi waliosajiliwa imeongezeka kutoka 69 mwaka 2020 hadi kufikia 338 mwaka 2024
Ameeleza pia serikali imeendelea na ujenzi wa barabara kwenye maeneo ambayo yana changamoto ya kufikika ili kurahisisha safari ya kutoka na kwenda kwenye vituo vya afya
Kuhusu mimba za utotoni ameeleza kuwa zimepungua kutoka 27% hadi kufikia 22%. Ameeleza pia lengo ni kuongeza umri wa kuishi (life expectancy) hadi kufikia angalau miaka 75.
Tuzo ya Gates Foundation Goalkeeper ilianzishwa mwaka 2017 chini ya Bill and Melinda Gates Foundation. Lengo kuu la tuzo hii ni kuchochea juhudi za kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) duniani.
Miongoni mwa washindi wa tuzo hii katika miaka iliyopita ni:
- Mwaka 2020: John Nkengasong, mtaalamu wa virusi na afya ya umma kutoka Cameroon.
- Mwaka 2021: Phumzile Mlambo-Ngcuka, mwanasiasa wa Afrika Kusini na afisa mwandamizi wa zamani wa Umoja wa Mataifa.
- Mwaka 2022: Ursula von der Leyen, Rais wa Tume ya Ulaya.
- Mwaka 2024: Luiz Inácio Lula da Silva, Rais wa Brazil.
Kwa muktadha huo, ni heshima ya kipekee kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutunukiwa tuzo hii, ikithibitisha mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ndani na nje ya Tanzania.
Rais Samia Suluhu Hassan:
Nikiwa ni Mwanamke na mama, nimepitia yale ambayo wanawake wengine wanapitia wakati wa uzazi.
Niliona kilichokuwa kikitokea katika Wadi za Wazazi, nimeona watu wanavyopita wakati mgumu wakati wa mchakato wa kujifungua kiasi kwamba wengine walipoteza maisha wakati wa mchakato, hiyo imechangia mimi kuwekeza katika suala la Afya hasa inayohusu mama na mtoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award kutoka kwa Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dkt. Anita Zaidi kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025. Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Mhe. Rais Samia amepewa Tuzo hiyo katika kipengele cha mapambano dhidi ya vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates kutoka Marekani Dkt. Anita Zaidi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Viongozi mbalimbali kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kimataifa ya The Global Goalkeepers Award kutoka Taasisi ya Gates ya Marekani. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025.
Tuzo Hii Muhimu itaendelea:-
1. kuithibitishia Dunia namna uongozi wake wa kipekee unavyotambulika katika kutekeleza sera na mipango inayolingana na malengo ya Bill & Melinda Gates Foundation, hasa katika kuboresha matokeo ya afya na elimu nchini Tanzania.
2. Kuonyesha Mchango wake mkubwa katika Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vitendo.
3. Kudhihiisha Namna Uongozi wake Mhe unavyoacha alama na kuleta mapinduzi makubwa kwa maisha ya Watanzania, hususan katika maeneo ya afya ya mama na mtoto, upatikanaji wa elimu, na kupunguza umasikini.
4. Tuzo hii itachochea viongozi wengine na wadau mbalimbali nchini Tanzania na maeneo mengine kuweka msukumo na kipaumbele kwenye mipango muhimu kama afya na mingine.
5. Itasaidia pia kuleta fursa nyingine zaidi ikiwemo Msaada. Aidha, kuendelea kuzidi Kutambuliwa huku kutaongeza na kuzidi kuing’arisha taswira ya Tanzania kimataifa, na hatimaye kuvutia ushirikiano zaidi, misaada na kupata miradi ya ziada ya maendeleo kwa Nchi yetu.