Rais Samia apewa Tuzo ya Gates Goalkeeper Award

Rais Samia apewa Tuzo ya Gates Goalkeeper Award

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Amepokea Tuzo ya Gates Goalkeeper Awards Hyatt Regency Hotel Dar es salaam, leo tarehe 04 Februari, 2025.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo ametoa hutoba ambapo Rais Samia ameeleza kuwa idadi ya wataalamu wa afya hususani wa afya ya uzazi waliosajiliwa imeongezeka kutoka 69 mwaka 2020 hadi kufikia 338 mwaka 2024

Ameeleza pia serikali imeendelea na ujenzi wa barabara kwenye maeneo ambayo yana changamoto ya kufikika ili kurahisisha safari ya kutoka na kwenda kwenye vituo vya afya

Kuhusu mimba za utotoni ameeleza kuwa zimepungua kutoka 27% hadi kufikia 22%. Ameeleza pia lengo ni kuongeza umri wa kuishi (life expectancy) hadi kufikia angalau miaka 75.

Tuzo ya Gates Foundation Goalkeeper ilianzishwa mwaka 2017 chini ya Bill and Melinda Gates Foundation. Lengo kuu la tuzo hii ni kuchochea juhudi za kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) duniani.

Miongoni mwa washindi wa tuzo hii katika miaka iliyopita ni:
  • Mwaka 2020: John Nkengasong, mtaalamu wa virusi na afya ya umma kutoka Cameroon.
  • Mwaka 2021: Phumzile Mlambo-Ngcuka, mwanasiasa wa Afrika Kusini na afisa mwandamizi wa zamani wa Umoja wa Mataifa.
  • Mwaka 2022: Ursula von der Leyen, Rais wa Tume ya Ulaya.
  • Mwaka 2024: Luiz Inácio Lula da Silva, Rais wa Brazil.
Tuzo hii inachukuliwa kuwa ya heshima kubwa duniani, na hafla ya utoaji wake hufanyika jijini New York, kwenye ukumbi wa Lincoln Center, mara nyingi sambamba na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA).

Kwa muktadha huo, ni heshima ya kipekee kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutunukiwa tuzo hii, ikithibitisha mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ndani na nje ya Tanzania.



Rais Samia Suluhu Hassan:
Nikiwa ni Mwanamke na mama, nimepitia yale ambayo wanawake wengine wanapitia wakati wa uzazi.

Niliona kilichokuwa kikitokea katika Wadi za Wazazi, nimeona watu wanavyopita wakati mgumu wakati wa mchakato wa kujifungua kiasi kwamba wengine walipoteza maisha wakati wa mchakato, hiyo imechangia mimi kuwekeza katika suala la Afya hasa inayohusu mama na mtoto.
WhatsApp Image 2025-02-04 at 15.06.23_6897a2d6.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award
WhatsApp Image 2025-02-04 at 15.05.42_1294c2cb.jpg

WhatsApp Image 2025-02-04 at 15.05.47_a29848e5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award kutoka kwa Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dkt. Anita Zaidi kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025. Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Mhe. Rais Samia amepewa Tuzo hiyo katika kipengele cha mapambano dhidi ya vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano.
WhatsApp Image 2025-02-04 at 15.05.56_7b594a99.jpg

WhatsApp Image 2025-02-04 at 15.05.51_e4d05a35.jpg

WhatsApp Image 2025-02-04 at 15.06.05_d4fa17e7.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates kutoka Marekani Dkt. Anita Zaidi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Viongozi mbalimbali kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kimataifa ya The Global Goalkeepers Award kutoka Taasisi ya Gates ya Marekani. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025.
WhatsApp Image 2025-02-04 at 15.06.15_6b554caf.jpg
Tuzo hiyo ya Gates Foundation Goalkeeper itaithibitishia Dunia umuhimu mkubwa kuhusu juhudi na kazi kubwa ambayo Rais Samia ameifanya katika kushughulikia changamoto za kimataifa, hasa katika afya na mengineyo.

Tuzo Hii Muhimu itaendelea:-
1.
kuithibitishia Dunia namna uongozi wake wa kipekee unavyotambulika katika kutekeleza sera na mipango inayolingana na malengo ya Bill & Melinda Gates Foundation, hasa katika kuboresha matokeo ya afya na elimu nchini Tanzania.

2. Kuonyesha Mchango wake mkubwa katika Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vitendo.

3. Kudhihiisha Namna Uongozi wake Mhe unavyoacha alama na kuleta mapinduzi makubwa kwa maisha ya Watanzania, hususan katika maeneo ya afya ya mama na mtoto, upatikanaji wa elimu, na kupunguza umasikini.

4. Tuzo hii itachochea viongozi wengine na wadau mbalimbali nchini Tanzania na maeneo mengine kuweka msukumo na kipaumbele kwenye mipango muhimu kama afya na mingine.

5. Itasaidia pia kuleta fursa nyingine zaidi ikiwemo Msaada. Aidha, kuendelea kuzidi Kutambuliwa huku kutaongeza na kuzidi kuing’arisha taswira ya Tanzania kimataifa, na hatimaye kuvutia ushirikiano zaidi, misaada na kupata miradi ya ziada ya maendeleo kwa Nchi yetu.
 
"Gates" ina uhusiano na Bill Gates ambaye huko kwao yeye Ford, George Soros,et al wamechafuka vibaya Sana?

Sijasoma hata Uzi maana Trump na Elon wamefichua upuuzi mwingi wa hawa mumiani....
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akipokea Tuzo ya Gates Goalkeeper Awards Hyatt Regency Hotel Dar es salaam, leo tarehe 04 Februali, 2025.


Kuhusu Gates Foundation Goalkeeper award at Hyatt This award started in 2017 under Bill and Melinda Gates Foundation. Dhumuni kubwa kuchochea dunia ikamilishe/ifanikishe SDGs. Past winners, in 2020 John Nkengasong Cameroonian virologist and public health expert, 2021 Phumzile Mlambo Ngcuka South African politician and former UN senior staff, 2022 Ursula von Der Leyen, President of the European Commission and in 2024 Luiz Inaco Lula da Silva President of Brazil. It's quite a prestigious award, usually the event takes place in NY during UNGA, Lincoln Hall. Hivyo ni heshima kubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kupokea tuzo hii.

Wana kitu wanataka kuomba hapa,nawaambia huyu mtu anaipeleka chi kubaya
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award
Gi8SMTiXEAAtvBF.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper AwardView attachment 3225136


Sikuhizi kuna tunzo za kila aina ndugu tusipotezeane muda. Kuna wanajeshi wamekufa sisi tunaona powa tu. Hatuwezi kuwa na nchi ya kusifiana sifiana kila siku wakati ukweli mambo sio hivyo. Misaada imekatwa huko ya USAID serekali kama haiwahusu wakati hatujui dawa sasa zitapatikana vipi, wanajeshi wanakufa hatujui plan zozote. Raisi anataka kwenda kusheherekea kupitishwa kuwa mgombea na wakina baba levo! Dodoma. Kapitishwa na Kikwete sasa sherehe za nini wakati wanajeshi wanakufa na hatuna plan za madawa. Sherehe kila siku. Mama Mama ....kama ni kuombewa tuombewe kwa kweli
 
👏🏽👏🏽👏🏽
🎊🎊🎊
Kazi iendeleeeee

Trump atamwonea wivu 🤗
 
Sikuhizi kuna tunzo za kila aina ndugu tusipotezeane muda. Kuna wanajeshi wamekufa sisi tunaona powa tu. Hatuwezi kuwa na nchi ya kusifiana sifiana kila siku wakati ukweli mambo sio hivyo. Misaada imekatwa huko ya USAID serekali kama haiwahusu wakati hatujui dawa sasa zitapatikana vipi, wanajeshi wanakufa hatujui plan zozote. Raisi anataka kwenda kusheherekea kupitishwa kuwa mgombea na wakina baba levo! Dodoma. Kapitishwa na Kikwete sasa sherehe za nini wakati wanajeshi wanakufa na hatuna plan za madawa. Sherehe kila siku. Mama Mama ....kama ni kuombewa tuombewe kwa kweli
Kesho ukifa wewe hakuna hata anaeshtuka emu amka usingizini huko kumekucha
 
Sikuhizi kuna tunzo za kila aina ndugu tusipotezeane muda. Kuna wanajeshi wamekufa sisi tunaona powa tu. Hatuwezi kuwa na nchi ya kusifiana sifiana kila siku wakati ukweli mambo sio hivyo. Misaada imekatwa huko ya USAID serekali kama haiwahusu wakati hatujui dawa sasa zitapatikana vipi, wanajeshi wanakufa hatujui plan zozote. Raisi anataka kwenda kusheherekea kupitishwa kuwa mgombea na wakina baba levo! Dodoma. Kapitishwa na Kikwete sasa sherehe za nini wakati wanajeshi wanakufa na hatuna plan za madawa. Sherehe kila siku. Mama Mama ....kama ni kuombewa tuombewe kwa kweli
Kliniki za kutoka ARV huku vijijini Leo siku ya pili hakuna huduma, watumishi walikuwa chini ya NGO ambayo ni wanufaika wa USAID nasikia Jana waliaga Hadi hapo mambo yakikaa Sawa...Sisi tupo tunapokea tuzo za kijinga "kaseja award'
 
wewe je umechagia nini kwa jamii. Hata mada za maana huna. Mimi ni mtu wewe ni mdudu chawa
Ukifa kesho utaambiwa kufa kwako hakuna faida kifo chako ni kifo tu yaan wewe ulistahiri kufa tu
 
Back
Top Bottom