Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Leo, Juni 10, 2025, Rais Samia amepokea gawio nono la Shilingi Trilioni 1.28, michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma, ikiwa ni ongezeko la asilimia 68. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam.
"Mbele yako leo hii Mhe. Rais ninayofuraha ya kukukabidhi Gawio ambalo ni nono kuliko la mwaka jana na kwamba mpaka kufikia jana (Juni 9,2025) Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanikiwa kukusanya kiasi cha TSh. Trilioni 1.28"
Fuatilia hapa: Rais Samia akipokea Gawio na Michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma Juni 10, 2025
Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema kiwango hiki ni ongezeko la asilimia 68 ikilinganishwa na Gawio la mwaka jana na alichokipokea leo.
Mchechu amesema, TSh 603.4 bilioni sawa na asilimia 59 ya gawio hilo zinatokana na mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache na TSh 363.4 zinatokana na mashirika yasiyozalisha faida na TSh21 bilioni zinatokana na vyanzo mbalimbali.
Kundi la 1: Taasisi na Mashirika ya Biashara ambayo yametoa Gawio zaidi ya TSh. Bilioni 10

- Twiga Minerals Corporation - Bil. 93.6
- Airtel Tanzania - Bil. 73.9
- Benki ya NMB - Bil. 68.1
- Puma Energy - Bil. 13.5
- TPDC - Bil. 11.7
- Benki ya NBC - Bil. 10.5
- Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) - Bil. 181.5
- Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) - Bilioni 38.8
- Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) - Bilioni 29.8
- Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) - Bilioni 20.4
- Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) - Bilioni 19.2
- Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) - Bilioni 16.3
- Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini (OSHA) - Bilioni 10.4