Rais Samia apokea gawio nono la Tsh. Tril 1.28, ongezeko la 68% kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma

Rais Samia apokea gawio nono la Tsh. Tril 1.28, ongezeko la 68% kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma

Kuna breakdown ya Gawio kutoka kwenye kila taasisi, tuanzie hapo Kwanza.

Maana unaweza kuambiwa ATCL imetoa gawio halafu huku kwa CAG unakuta ATCL hiyo imepata hasara.
 
Kazi nzuri ya Mageuzi aliyoifanya Sasa inaleta faida.

Hasara zimepungua yamesalia mashirika chini ya 5 yanayopata hasara ambao ni TTCL,ATCL,Tazara,TRC
ATCL haina hasara kwa maana ile tunayoifahamu, pesa iliwekezwa nyingi na huchukua miaka kadhaa kuweza faida kuonekana. Ni vigumu kwa shirika la ndege kutengeneza faida ndani ya muda mfupi tukizingatia hapo kabla shirika lilikuwa na madeni mengi.
 
Hivi hawawezi kupeana tu haya matrilioni juu kwa juu kwenda hazina bila kufanya masherehe kama haya? Huyu jamaa angempelekea mama cheque tu pale ikulu au wire transfer advice isingekua sawa tu!
 
Kwa sisi wahasibu lazima tuzione AFS za hizo taasisi zilizotoa gawio, je kulikuwana any accumulated profit ambayo gawio limeithinishwa , na ni shilingi ngapi kwakila mwanhisa

zisije zikawa ni gawio kiini macho na hakuna chochote
 
Leo, Juni 10, 2025, Rais Samia amepokea gawio nono la Shilingi Trilioni 1.28, michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma, ikiwa ni ongezeko la asilimia 68. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam.

"Mbele yako leo hii Mhe. Rais ninayofuraha ya kukukabidhi Gawio ambalo ni nono kuliko la mwaka jana na kwamba mpaka kufikia jana (Juni 9,2025) Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanikiwa kukusanya kiasi cha TSh. Trilioni 1.28"

Fuatilia hapa: Rais Samia akipokea Gawio na Michango kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma Juni 10, 2025

Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema kiwango hiki ni ongezeko la asilimia 68 ikilinganishwa na Gawio la mwaka jana na alichokipokea leo.

Mchechu amesema, TSh 603.4 bilioni sawa na asilimia 59 ya gawio hilo zinatokana na mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache na TSh 363.4 zinatokana na mashirika yasiyozalisha faida na TSh21 bilioni zinatokana na vyanzo mbalimbali.

Kundi la 1: Taasisi na Mashirika ya Biashara ambayo yametoa Gawio zaidi ya TSh. Bilioni 10
  • Twiga Minerals Corporation - Bil. 93.6
  • Airtel Tanzania - Bil. 73.9
  • Benki ya NMB - Bil. 68.1
  • Puma Energy - Bil. 13.5
  • TPDC - Bil. 11.7
  • Benki ya NBC - Bil. 10.5
Kundi la 2: Taasisi zinazotoa asilimia 15 ya mapato ghafi
  • Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) - Bil. 181.5
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) - Bilioni 38.8
  • Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) - Bilioni 29.8
  • Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) - Bilioni 20.4
  • Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) - Bilioni 19.2

Wakati wa Jiwe, gawio lilitolewa na mashirika/taasisi ambayo yalikuwa yanapata hasara, na zaidi wengine walikopa ili watoe gawio.

Sifa za kijinga hazitakiwi.
Reflection ya faida ya hayo mashirika inabidi ionekane katika jamii, na sio kusikia tuu wanatoa gawio kwa kupata faida.

TFS na NIDA wanawapita TANAPA!!!!???
Uvunaji wa Carbon ndio unawabeba TFS!!!??
NIDA jee!!!???
 
NIDA wanapata wapi faida? Navyofahamu vitambulisho ni bure, any explanation?
 
Mapato yanapanda yet Mambo kitaa yanazidi kuwa magumu...; Labda kipaumbele kwa mashirika hayo yangekuwa ni kutoa huduma kwanza kabla ya kuwaza kukusanya hizo so called Gawio (Hao NIDA wapo busy kutoa Gawio wakati watu hawana Vitambulisho na wanaopewa hivyo vitambulisho vinafutika vikipigwa upepo)


 
Ni wazi Kwa gawio alilopokea Samia anaenda kuwa tajiri wa Taifa.
 
Emu wajuzi wa mambo mtupe Elimu kidogo.
Hayo mashirika ambaya hayazalishi faida yanapata wapi pesa za kutoa kama gawio kwa serikali!??
 
Ripoti ijayo ya CAG tutarajie faida tupu na sio hasara tena😁😁😁
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Gawio la Serikali kutoka Mashirika ya Umma na Taasisi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Gawio la Serikali kutoka Mashirika ya Umma na Taasisi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Dar es Salaam, 10 Juni 2025: Hatua madhubuti za mageuzi zilizoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, zimeanza kuzaa matunda makubwa baada ya Serikali kupokea gawio na michango mingine ya kihistoria ya Sh1.028 trilioni kutoka kwa mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa.

Takwimu hizi ni matokeo ya utekelezaji wa mikakati ya kuongeza tija na ufanisi katika utendaji wa taasisi, ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Samia kuhusu uwajibikaji na ufanisi wa taasisi za umma tangu alipoingia madarakani.


Akizungumza katika tukio hilo maalumu la “Gawio Day”, Rais Samia alisema kuwa makusanyo hayo ni ishara ya mabadiliko ya kiutendaji yanayolenga kujenga taasisi imara, zenye uwezo wa kujitegemea na kuchangia kikamilifu maendeleo ya Taifa.

“Nimefurahishwa sana na ongezeko hili la mapato lisilo na mfano tangu kuanzishwa kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina mwaka 1959. Hii ni hatua kubwa katika safari yetu ya mageuzi,” alisema Rais Samia.

Ameongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo, bado Serikali ina malengo makubwa zaidi — ikiwemo kuvuka kiwango cha Sh1.5 trilioni kwa mwaka ujao — ikiwa ni sehemu ya dira ya kujenga mashirika yenye ufanisi mkubwa, yanayochochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.


Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, mafanikio haya yametokana na ufuatiliaji makini, usimamizi thabiti, pamoja na utekelezaji wa falsafa ya Rais ya “R4”, hususan kipengele cha “Reforms and Rebuild”.

Katika msisitizo wa mageuzi zaidi, Mhe. Rais ametoa maagizo manne muhimu kwa taasisi ikiwemo: ubunifu katika kutatua changamoto na kuongeza tija, kukamilisha sheria ya uwekezaji wa Umma, kuimarisha mifumo ya TEHAMA kwa ufanisi zaidi, na kuwajengea watumishi uwezo na kutoa motisha stahiki.

“Tusisubiri kila tatizo kutatuliwa na Serikali. Tuwe wabunifu, tutumie fursa kama soko la mitaji kuboresha utendaji wetu,” alisema Rais Samia huku akiwataka viongozi wote wa taasisi kushiriki kikamilifu katika safari ya mageuzi.
_DSC5943.jpg

Kampuni ya Puma Energy Tanzania haikubaki nyuma katika mchakato huu kwani ilichangia kiasi cha shilingi bilioni 13 kama gawio.

Akizungumza mara baada ya hafla hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bi. Fatma Abdalla alisema, “Tunajivunia kuwa sehemu ya tukio hili la kihistoria kwa taifa. Mchango wetu unaakisi uwazi, ubora wa utendaji, na dhamira ya Puma Energy Tanzania katika kuiunga mkono Tanzania yenye ajenda ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.”

Katika mwaka wa fedha 2024/25, taasisi 213 zimechangia Sh1.028 trilioni, sawa na ongezeko la asilimia 68 ukilinganisha na mwaka jana. Hii ni sehemu ya mafanikio yanayoimarisha msingi wa uchumi wa nchi kupitia mashirika binafsi.
​
 
Serikali imepokea gawio la jumla ya Shilingi Trilioni 1.028, ikiwa ni ongezeko la asilimia 34 ikilinganishwa na Shilingi Bilioni 767 zilizokusanywa mwaka 2024.
 
NIDA wanapata wapi faida? Navyofahamu vitambulisho ni bure, any explanation?
Mabank, makampun ya Simu na taasis nyingi kama NHIF ambazo huwa wanahitaji Namba ya NIDA kwenye kupata huduma wanachukua data NIDA kupitia kuunganisha mifumo yao na NIDA ..taasis hizo zote zinalipia hiyo huduma na ni hela nzuri tuu wanatoa
 
Back
Top Bottom