Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kazi nzuri ya Mageuzi aliyoifanya Sasa inaleta faida.Hii leo Rais Samia amepokea gawio nono la TSh. Trilioni 1.28, Michango kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma, Ongezeko la asilimia 68
View attachment 3363018
Taasisi zote zinaleta faida kama wakiamua ,nyingi sana..Wakiweza waziunganishe ila hasara zinatoka na siasa tu.Taasisi gani imeleta faida? Tupo pazuri
Walizoiba nyingi kuliko hilo igizo la gawioMabilionea wataongezeka.....
Walishapiga kubwa kabla, hapo wanafanya maigizo tupu80% inaenda kwenye kampeni ..10% mifukoni, 10% kupambana na upinzani.
80% inaenda kwenye kampeni ..10% mifukoni, 10% kupambana na upinzani.
Hili ndiyo gawio la kweli hapa hatanii
Ubunifu umeanza kuzaa matunda. Gooooood job!Leo, Juni 10, 2025, Rais Samia amepokea gawio nono la Shilingi Trilioni 1.28, michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma, ikiwa ni ongezeko la asilimia 68. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam.
"Mbele yako leo hii Mhe. Rais ninayofuraha ya kukukabidhi Gawio ambalo ni nono kuliko la mwaka jana na kwamba mpaka kufikia jana (Juni 9,2025) Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanikiwa kukusanya kiasi cha TSh. Trilioni 1.28"
Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema kiwango hiki ni ongezeko la asilimia 68 ikilinganishwa na Gawio la mwaka jana na alichokipokea leo.
Mchechu amesema, TSh 603.4 bilioni sawa na asilimia 59 ya gawio hilo zinatokana na mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache na TSh 363.4 zinatokana na mashirika yasiyozalisha faida na TSh21 bilioni zinatokana na vyanzo mbalimbali.
Mashirika mengi yanakopa benki ili kutoa gawio kumridhisha Hangaya.View attachment 3363026
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amesema kwa mwaka huu mashirika na taasisi za Serikali wanatoa jumla Sh1.28 trilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 68 kulinganisha na gawio la mwaka 2024.
Akizungumza wakati wa kutoa gawio na mchango wa taasisi na mashirika ya umma, leo Juni 10 jijini Dar es Salaam
mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, Mchechu amesema, Sh603.4 bilioni sawa na asilimia 59 ya gawio hilo zinatokana na mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache na Sh363.4 zinatokana na mashirika yasiyozalisha faida na Sh21 bilioni zinatokana na vyanzo mbalimbali.
Fuatilia:
Rais Samia akipokea gawio na mchango wa mashirika ya umma na taasisi za Serikali
Gawio nene na hapo hapo mnazidi kukopa nje na ndani!Gwio Nono wakati Deni la Taifa linaongezeka kwa speed ya 10G, Nonsense.
No Reform No Election!!!