Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
RAIS SAMIA APONGEZA KUANZISHWA KWA KITUO JUMUISHI MAHUSUSI KWA KUSHUGULUKIA MASHAURI YA KIFAMILIA
Na Mwandishi Wetu
06/10/2021
🇹🇿🇹🇿
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi hizo leo Jijini Dodoma wakati akizindua vituo jumuishi vya utoaji haki.
Mahakama Kuu imeanzisha kituo jumuishi ambacho kitakuwa mahususi kwa ajili ya mashitaka ya kifamilia, mashitaka hayo ni yale yanayohusu mirathi, ndoa,talaka, malezi na matunzo ya watoto na haki zao pia.
Hii imekuja baada ya kesi zinazohusu familia kuwa nyingi katika jamii na kuchukua muda mrefu hadi kumalizika kwake, hivyo kupelekea haki kuchelewa.
Kituo hiki kinaitwa "Kituo jumuishi" kwa sababu kuu ya kwamba, kutakuwa na kila ofisi ya kimahakama, ambapo haki itapatikana ndani ya muda mfupi. Lakini pia hata ukataji wa rufaa wa kesi utakuwa ndani ya jengo moja.
Kwa Jiji la Dar es Salaam mahakama hii itakuwepo Temeke, na baadae kusambaa katika Kanda zote za Mikoa ya Tanzania.
Mhe Rais ameipongeza kwa dhati mahakama kwa kuliona hili suala kesi za kifamilia kuchelewa kumalizika kwake na kupelekea haki kupotea, Jambo ambalo ni kero kubwa katika jamii yetu ya watanzania.
Mahakama kuja na suluhusho la kuanzisha kituo kimoja kitakacho kuwa na vitengo vyote vya kutoa haki katika sehemu moja ni jambo jema sana lenye kupongezwa na kila mtu.
🇹🇿🇹🇿
#TwendePamoja
#KwaMatokeoYaHaraka