Rais Samia Apongezwa kwa kuwa mfano bora kwa Wanawake

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Rais Samia Apongezwa kwa kuwa mfano bora kwa Wanawake

Wanawake wa Taasisi ya Salama Mapesa kutoka mji wa Ntsoudjini wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na kupongeza uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kiongozi mfano bora kwa wanawake Afrika.

Viongozi wa Taasisi hiyo walifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu pia walimueleza hamu yao ya kushirikiana na Taasisi za Wanawake nchini Tanzania hasa katika maeneo ya Ujasiriamali, Mafunzo ya Vitendo na Utamaduni.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Bi. Farida Madi alieleza kuwa wanaona uhusiano umeimarika kati ya Tanzania na Comoro katika kipindi cha uongozi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Azali Assoumani na wangependa taasisi yao kupata mshirika wa kufanya naye kazi Tanzania hasa katika maeneo ya mafunzo kwa wasichana, utamaduni kwa kuwa Taasisi yao pia inajishughulisha na kuienzi ngoma ya Lele Mama nchi Comoro.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Yakubu aliwashukuru kwa pongezi hizo na kuwaahidi kuwaunganisha na Taasisi za Maendeleo ya Wanawake nchini Tanzania.

IMG-20250612-WA0059.jpg
IMG-20250612-WA0061.jpg
IMG-20250612-WA0060.jpg
 
Attachments

  • IMG-20250612-WA0062.jpg
    IMG-20250612-WA0062.jpg
    1.2 MB · Views: 28
Rais Samia Apongezwa kwa kuwa mfano bora kwa Wanawake

Wanawake wa Taasisi ya Salama Mapesa kutoka mji wa Ntsoudjini wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na kupongeza uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kiongozi mfano bora kwa wanawake Afrika.

Viongozi wa Taasisi hiyo walifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu pia walimueleza hamu yao ya kushirikiana na Taasisi za Wanawake nchini Tanzania hasa katika maeneo ya Ujasiriamali, Mafunzo ya Vitendo na Utamaduni.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Bi. Farida Madi alieleza kuwa wanaona uhusiano umeimarika kati ya Tanzania na Comoro katika kipindi cha uongozi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Azali Assoumani na wangependa taasisi yao kupata mshirika wa kufanya naye kazi Tanzania hasa katika maeneo ya mafunzo kwa wasichana, utamaduni kwa kuwa Taasisi yao pia inajishughulisha na kuienzi ngoma ya Lele Mama nchi Comoro.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Yakubu aliwashukuru kwa pongezi hizo na kuwaahidi kuwaunganisha na Taasisi za Maendeleo ya Wanawake nchini Tanzania.
Acha usseng..
 
Siku hizi uchawa umevuka border...!Kuna hadi uchawa wa kimataifa!
 
Back
Top Bottom