Rais Samia asema bima ya afya kwa wote ni jambo zito si jambo jepesi

Rais Samia asema bima ya afya kwa wote ni jambo zito si jambo jepesi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Rais Samia Suluhu Hassan amesema mpango wa kuwa na bima ya afya kwa wote ni mzito na si mwepesi kutokana na umuhimu wake.

Pia, kuhusu suala hilo amelishukuru Bunge kwa kulipitisha huku akisema kwa sasa limebaki upande wa Serikali kulifanyia kazi.

"Jambo hili ni zito na sio jepesi, tunalishukuru Bunge kwa kulipitisha, kwa sasa limebaki upande wetu (Serikali), tunakwenda tunajaribu halafu tunarudi kurekebisha,"amesema Rais Samia.

Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Machi 8, 2025 akihutubia katika Siku ya Wanawake Duniani inayofanyika kitaifa mkoani Arusha.

"Tunataka kila Mtanzania awe na bima ya afya ili tuweze kudhibiti na kulinda hadhi ya huduma za afya tuliyonayo," amesema.

 
Lakini Kununua Mabasi,,,Mabango Nchi Nzima,,Machapisho,,Vipeperushi n.k,n.k Ni Jambo Jepesi Kwa Simba Sports Club
 
Back
Top Bottom