Vyanzo vya maji kwa ajili ya umwagiliaji ni vingi mkuu.
1. Mvua (muda ambao inanyesha, unajenga mifereji kuyapeleka maji shambani)
2. Kuvuna maji ya mvua na kuyaweka kwenye mabwawa makubwa ili baadae uyapeleke shambani. (Kutoyaacha maji ya mvua "yaende zake")
3. Kuchimba maji ya chini (underground water) na kuya pump kwenda shambani.
4. Na njia nyinginezo.
Sidhani kama options zote hizo zinashindikana kwa Dodoma (au eneo jingine lolote).
Kama Dodoma inasifika kwa kilimo cha zabibu, maana yake to some point Dodoma inapata maji ambayo mnaweza kuya utilise kwa ajili ya umwagiliaji.
Vinginevyo tukubaliane kwamba hata hizo zabibu zinakua kwa NGUVU YA UPEPO