Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Kikagati Murongo, Uganda, leo Mei 25, 2023.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemshukuru Rais Samia kwa kuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika eneo hilo. Amesema alipanga kuonana na marais wengine wa Tanzania lakini kutokana na sababu mbalimbali hakufanikiwa.
Akizungumza kwenye halfa hiyo, Rais Samia amempongeza Rais Museveni kwa mradi huo na ameshukuru kwa uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uganda kwenye nyanja mbalimbali ambapo mradi huu utaongeza zaidi ushirikiano huo.
Rais Samia amesema umeme utakaozalishwa hapo utaongeza mashirikiano ya kibiashara, usafirishaji wa watu na bidhaa, afya, veta na mengine kadhalika.
Umeme huu utawakutanisha zaidi watu pamoja na kuongeza ulinzi wa maeneo ya nchi hizi kwa kuunganisha maeneno ya mijini na vijjini.
Ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itafanya kila linalowezekana kufanya mradi huu uendelee bila vikwazo. Pia, ipo tayari kwa mradi huu kwa kuwa inawekeza sana kwenye kusambaza umeme vijijini, na vyanzo vya aina hii vya umeme vinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza lengo hilo ya Serikali.
Akielezea zaidi kuhusu mradi huo na eneo uliopo, Rais Museveni amesema yeye binafsi amezaliwa na kukulia karibu na eneo hilo, amepigana vita 3 kwenye eneo hilo na amechunga ng'ombe upande wa Tanzania.
Amewataka Waganda kutokusikitika baada ya kusikia Tanzania inautaka umeme, amehoji Waganda wanasikitika na kunung'unika kwa kipi wakati Umeme huo hautolewi bure? Hata kama wataununua wote Nchi yake itapata pesa na hakutakuwa na tatizo lolote.
Wazo la mradi huo mara kwa kwanza Rais Museveni alimshirikia Hayati Magufuli ambaye aliukubali, na Rais Samia alipoingia madarakani hakusika kuuendeleza.
Rais Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda Mei 25, 2023. Mradi huo wa umeme utanufaisha nchi zote mbili katika masuala ya Nishati ya umeme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.
Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati wakisikiliza maelezo ya mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.