Rais Samia ashiriki Hafla ya uzinduzi wa Mradi wa kufua Umeme wa Kikagati Murongo, Uganda, Mei 25, 2023

Rais Samia ashiriki Hafla ya uzinduzi wa Mradi wa kufua Umeme wa Kikagati Murongo, Uganda, Mei 25, 2023

Nimeishi pale murongo kwakweli wanakijiji watanufaika I'la hapo hapo wenzetu Uganda mtambo wao nimkubwa walituwahi kutangulia kujenga kwakuwa uzalishaji umeweka jirani jirani lingekuwa sisi wenyewe tungepata kv nyingi
Mkuu unajua lemira na isuki??
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Kikagati Murongo, Uganda, leo Mei 25, 2023.



Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemshukuru Rais Samia kwa kuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufika eneo hilo. Amesema alipanga kuonana na marais wengine wa Tanzania lakini kutokana na sababu mbalimbali hakufanikiwa.

Akizungumza kwenye halfa hiyo, Rais Samia amempongeza Rais Museveni kwa mradi huo na ameshukuru kwa uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uganda kwenye nyanja mbalimbali ambapo mradi huu utaongeza zaidi ushirikiano huo.

Rais Samia amesema umeme utakaozalishwa hapo utaongeza mashirikiano ya kibiashara, usafirishaji wa watu na bidhaa, afya, veta na mengine kadhalika.

Umeme huu utawakutanisha zaidi watu pamoja na kuongeza ulinzi wa maeneo ya nchi hizi kwa kuunganisha maeneno ya mijini na vijjini.

Ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itafanya kila linalowezekana kufanya mradi huu uendelee bila vikwazo. Pia, ipo tayari kwa mradi huu kwa kuwa inawekeza sana kwenye kusambaza umeme vijijini, na vyanzo vya aina hii vya umeme vinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza lengo hilo ya Serikali.

Akielezea zaidi kuhusu mradi huo na eneo uliopo, Rais Museveni amesema yeye binafsi amezaliwa na kukulia karibu na eneo hilo, amepigana vita 3 kwenye eneo hilo na amechunga ng'ombe upande wa Tanzania.

Amewataka Waganda kutokusikitika baada ya kusikia Tanzania inautaka umeme, amehoji Waganda wanasikitika na kunung'unika kwa kipi wakati Umeme huo hautolewi bure? Hata kama wataununua wote Nchi yake itapata pesa na hakutakuwa na tatizo lolote.

Wazo la mradi huo mara kwa kwanza Rais Museveni alimshirikia Hayati Magufuli ambaye aliukubali, na Rais Samia alipoingia madarakani hakusika kuuendeleza.

View attachment 2634344
Rais Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda Mei 25, 2023. Mradi huo wa umeme utanufaisha nchi zote mbili katika masuala ya Nishati ya umeme.

View attachment 2634345
View attachment 2634346
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

View attachment 2634347
View attachment 2634348
View attachment 2634349View attachment 2634350
Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

View attachment 2634351
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati wakisikiliza maelezo ya mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Wababishaji wa kiswahili. Megawati 14 mirais miwili. Ingekuwa Japan kitu kama hii anafungua mkuu wa kitengo na watu wanaendelea na maisha. Shame on them.
 
Alipotaja jina la magufuli mlizionaje sura za viongozi wenza? walinuna, walicheka au walijikausha!!!! Mlio na tv mtusimulie
 
Yaani hujakaa na wataalamu wako, kuangalia mradi una athari gani kwa nchi yako, wewe unaamua tu kuwapa ruhusa watu wa nchi nyingine waweke mradi katika chanzo cha maji ya ziwa victoria!.
 
Yaani hujakaa na wataalamu wako, kuangalia mradi una athari gani kwa nchi yako, wewe unaamua tu kuwapa ruhusa watu wa nchi nyingine waweke mradi katika chanzo cha maji ya ziwa victoria!.
Ule mradi sisi tunafaidi kikubwa kwa maana mto sehemu kubwa maji yamelalia Uganda maporomoko yapo Uganda sehemu yetu kidogo sana na hujui mto kagera vizuri ule mto umekaa Uganda kikubwa kwetu umekuja kuingia Tanzania kidogo alafu kule mwisho ziwa Victoria mto umemwaga maji upande wa uganda ila pale mulongo sisi tunafaidi zaidi
 
Game reserves zipo upande wa Tz?

Ila wapo waganda na wa Tz wanaovuka ?
Ila game reserve upo upande wa Tanzania ukishapita mulongo custom watu wanavuka vizuri upande wa Uganda maduka makubwa na wenyeji ndiyo wengi na Barbara za lami wao sisi vumbi wenzetu wametupita parefu mkuu
 
Hiyo kofia aliyovaa mzee baba ni kofia ya chuma aseeee , ukilenga risasi inadunda
 
Hatimaye wana Murongo tumefikiwa. Tunakushukuru sana huu mradi kukamilika.
Ongeza minofu kidogo.
Mradi uligharimu kiasi gani. Hiyo pesa nayo ilikopwa?

Uganda wanatuuzia umeme, kwa hiyo ni mradi wa Uganda, au siyo?

Kuna mengi yasiyofahamika kuhusu huu mradi!

Ule mradi wa kule Rwanda na Burundi, mbona wenyewe haukamiliki? Ni siku nyingi sana tokea ujenzi wa mradi huo uanze, hadi leo umeme bado haujazalishwa, tatizo ni nini hasa? Huo mradi ni kama ule wa SGR ya Dar kwenda Morogoro! Stori chungu nzima, lakini hakuna kinachoonekana kikifanyika kuukamilisha.
 
The Kikagati Hydroeletric Power Project is a low-head, run-of-river 16 MW Hydroelectric Project on River Kagera.

The Kagera River is the main tributary to Lake Victoria and the river basin area lies within Rwanda, Burundi, Tanzania and Uganda.

The site is on the border between Uganda and Tanzania and includes dams and a short headrace and tailrace founded on largely varying ground conditions
Who 're the investors?
 
Who 're the investors?
NI Binafsi kwa sababu ni mradi mdogo. mdogo.
Kikagati is a 16 MW hydropower project in Uganda under development. Norfund has provided project development financing to the company.

KIKAGATI POWER COMPANY LTD​

 
Ila game reserve upo upande wa Tanzania ukishapita mulongo custom watu wanavuka vizuri upande wa Uganda maduka makubwa na wenyeji ndiyo wengi na Barbara za lami wao sisi vumbi wenzetu wametupita parefu mkuu
Mara nyingi boda zetu zisizokuwa na threat na faida huwa zinakuwa hovyo nilivyosikia
 
Back
Top Bottom