Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Kilele cha Maadhimisho ya Mbio za Mwenge katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini Mkoani Kagera leo tarehe 14 Oktoba, 2022
Hotuba ya Rais Samia
- Rais Samia ametoa salaam na Shukrani kwa Viongozi wote waliohudhuria pamoja na wananchi
Nawasifu na kuwapongeza vijana wetu sita wakiongozwa na kijana sahihi Nyanzabara Geraruma kwa kuukimbiza mwenge wa uhuru Tanzania nzima kuanzia tarehe 2 Aprili hadi leo tarehe 14 Oktoba na kwa kufuata misingi ile ile iliyowekwa na Waasisi wa taifa hili ya kuwahimiza Wananchi kudumisha uzalendo, umoja na mshikamano na kufanya kazi kwa bidii.
Ndugu wananchi kama mnavyofahamu Muasisi wetu Mlm Nyerere alipenda haki na usawa na alichukizwa na ukandamiazaji na dhuluma. Ni katika mantiki hiyo hiyo vijana wetu waliokimbiza mwenge walifanya kazi na kuelemisha mapambano dhidi ya dhuluma, ufisadi na rushwa. Walifanya kazi kurejeshwa jumla ya bilioni 2 milioni 200 zilizokopwa na vijana wengine na kupotea.
Pamoja na hawa lakini pia nawapongeza vijana wetu waliotoka Dar es Salaam mpaka Bukoba kwa miguu. Nawapongeza sana, huu ni uzalendo wamefanya kazi kubwa sana na wenyewe pia wanapaswa kutizamwa kwa jicho jema la rehema,.
Hivyo, siku ya leo sote tunawajibika kukumbuka mambo mema yaliyofanywa na Waasisi wetu Nyerere na Karume na urithi waliotuachia. Nami nitumie fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuendeleza na kuwaenzi wazee wetu hawa. kwa kufanya kazi, kuwa na mshikamano na uzalendo.
Amesema Vitendo vya Rushwa Vinajirudia kwa kuwa Viongozi katika maeneo mbalimbali hawafuatilii Maendeleo ya Miradi ya Wananchi hadi Mwenge unapopita na kubaini dosari.
Aidha, amewataka Viongozi na Watendaji kuhakikisha wanasimamia matumizi sahihi ya Fedha zinazoelekezwa katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Hotuba ya Rais Samia
- Rais Samia ametoa salaam na Shukrani kwa Viongozi wote waliohudhuria pamoja na wananchi
Nawasifu na kuwapongeza vijana wetu sita wakiongozwa na kijana sahihi Nyanzabara Geraruma kwa kuukimbiza mwenge wa uhuru Tanzania nzima kuanzia tarehe 2 Aprili hadi leo tarehe 14 Oktoba na kwa kufuata misingi ile ile iliyowekwa na Waasisi wa taifa hili ya kuwahimiza Wananchi kudumisha uzalendo, umoja na mshikamano na kufanya kazi kwa bidii.
Ndugu wananchi kama mnavyofahamu Muasisi wetu Mlm Nyerere alipenda haki na usawa na alichukizwa na ukandamiazaji na dhuluma. Ni katika mantiki hiyo hiyo vijana wetu waliokimbiza mwenge walifanya kazi na kuelemisha mapambano dhidi ya dhuluma, ufisadi na rushwa. Walifanya kazi kurejeshwa jumla ya bilioni 2 milioni 200 zilizokopwa na vijana wengine na kupotea.
Pamoja na hawa lakini pia nawapongeza vijana wetu waliotoka Dar es Salaam mpaka Bukoba kwa miguu. Nawapongeza sana, huu ni uzalendo wamefanya kazi kubwa sana na wenyewe pia wanapaswa kutizamwa kwa jicho jema la rehema,.
Hivyo, siku ya leo sote tunawajibika kukumbuka mambo mema yaliyofanywa na Waasisi wetu Nyerere na Karume na urithi waliotuachia. Nami nitumie fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuendeleza na kuwaenzi wazee wetu hawa. kwa kufanya kazi, kuwa na mshikamano na uzalendo.
RAIS SAMIA AAGIZA TAKUKURU NA ZAECA KUCHUNGUZA MIRADI ILIYOBAINIKA KUWA NA WIZI
Akihutubia Katika Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mkoani Kagera, Rais Samia ameziagiza Taasisi hizo za Kupambana na Rushwa kuwachukulia hatua Wasimamizi wa Miradi iliyobainika kuwa na Ufujaji, Wizi, Matumizi Mabaya ya Fedha, na Rushwa.Amesema Vitendo vya Rushwa Vinajirudia kwa kuwa Viongozi katika maeneo mbalimbali hawafuatilii Maendeleo ya Miradi ya Wananchi hadi Mwenge unapopita na kubaini dosari.