Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 leo tarehe 09 Desemba, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Kuacha kufanyika kwa sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ni sahihi?

View: https://www.youtube.com/live/wD6xPrxfO1M?si=evBA8PUCdgDxTepN

===

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameainisha changamoto zinazopaswa kupewa kipaumbele ikiwemo kufungamanisha ukuaji wa uchumi na sekta za uzalishaji. Rais Samia amesema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara sanjari na Mkutano wa kwanza wa uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Aidha Rais Samia ametaka sekta mbalimbali za uzalishaji ziimarishwe zaidi ikiwemo kilimo ambayo inakua kwa asilimia 4 tu kwa sasa tofauti na inavyotakiwa. Pia amesisitiza kuimarishwa kwa ushiriki wa sekta binafsi ndani na nje ya nchi ili kufanya wenyeji kuwa na utayari wa kupokea na kushirikiana na wageni wanaokuja kuwekeza na kufanya biashara nchini. Rais Samia amesema dira hiyo mpya itatakiwa kuzingatia kigezo cha kuongeza pato la kila mwananchi kufikia dola za Kimarekani 3,000 kwa mwaka ambacho hakikufikiwa katika dira ya mwaka 2000-2025.

Amesema kushindwa huko kulisababishwa na ukuaji wa uchumi kutojielekeza kwenye sekta zinazogusa maisha ya watu wengi, hivyo umasikini vijijini haujapungua kwa kasi iliyotarajiwa. Kuhusu suala la Maadili ya Taifa (ethos), Rais Samia amesema ni muhimu taifa kuwa na watu mahiri, makini na waadilifu ili kupata jamii inayochukia rushwa kila mahali, inayojituma na kufanya kazi bila kusukumwa na inayopinga na kulaani ukwepaji kodi.

Vile vile, Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania wote ndani na nje ya nchi (Diaspora) kushiriki kutoa maoni katika kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo kupitia njia za kisasa zitakazoainishwa na Tume ya Mipango.

Zuhura Yunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,

Ikulu
IMG_9303.jpeg

Huku Rais Samia Suluhu Hassan akizindua mpango wa ushirikishwaji wananchi katika maandalizi ya Dira ya maendeleo ya Mwaka 2025-2050 suala ambalo limewaibua wanasiasa wakisema mpango huo wa ushirikishwaji wa wananchi umekuja kwa kuchelewa
01000000-0a00-0242-7ed3-08dbf8e6206a_w1023_r1_s.jpeg

Watanzania wameadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika wakiwa na maoni mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya taifa hilo wakisema bado changamoto ni nyingi kwa wananchi ikilinganishwa na maendeleo yanayozungumziwa na viongozi.

Huku Rais Samia Suluhu Hassan akizindua mpango wa ushirikishwaji wananchi katika maandalizi ya Dira ya maendeleo ya Mwaka 2025-2050 suala ambalo limewaibua wanasiasa wakisema mpango huo wa ushirikishwaji wa wananchi umekuja kwa kuchelewa.

Wananchi hao wamesema wakati taifa hilo likiadhimisha miaka 62 ya uhuru bado maendeleo yamekuwa yanaonekana kwenye baadhi ya maeneo huku changamoto zikiwa ni nyingi ukilinganisha na maendeleo yaliyopatikana.

Anikazi Kumbemba mkazi wa Shinyanga anasema bado hali ya mwananchi mmoja mmoja kiuchumi haijaimarika kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi hao bado wanaishi kwenye umaskini.

“Bado hatujawasaidia Watanzania kwasababu hata hali zao kimaisha bado ni changamoto lakini maendeleo ya miundombinu tumejitahidi kwa kiasi chake lakini kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja bado tuna changamoto kubwa sana miaka hii 62 ya uhuru wa Tanganyika” amesema Kumbemba.
01000000-0a00-0242-b757-08dbf8e5bcae_w650_r1_s.jpeg

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka wananchi

Katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru huko jijini Dodoma Rais Samia amezindua mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utakaowawezesha wananchi kutoa maoni yao juu ya Dira hiyo.

Suala ambalo wanasiasa wanaona limekuja kwa kuchelewa kwa kuwa Dira hiyo kwa asilimia kubwa imekwisha kuandikwa hivyo kushirikishwa kwa wananchi kwenye hatua hizo za mwisho ni kuwalaghai kama anavyoeleza Dkt Wilbroad Peter Slaa

“Mimi naona siyo kwamba wananchi wamechelewa kushirikishwa, hawajashirikishwa kinchofanyika hivi sasa ni namna ya kuwapamba tu wananchi kwamba watashirikishwa kwasababu huwezi kumshirikisha mtu ikiwa umekwisha andika asilimia kubwa ya Dira hiyo, utakuwa unakwenda kumshirikisha nini huyo mwananchi?”

Dira ya Taifa ni muhimu kwa mataifa yote duniani kwa kuwa ni mwongozo wa muda mrefu unaoweka malengo na matarajio ya maendeleo ya nchi kwa miaka mingi ijayo inajumuisha maono na malengo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa ambayo taifa linataka kufikia.

Dkt Vicent Stansilaus ambaye ni Mchumi na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu huria Tanzania anasema ni muhimu kwa taifa la Tanzania kukipa kipaumbele kilimo katika Dira ya maendeleo ya mwaka 2050 kwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.

Stanslaus anasema “Kama taifa tunategemea sana kilimo kiwe ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu kwasababu utakuta idadi kubwa ya Watanzania wanategemea kilimo kwahiyo ningetamani nguvu kubwa ielekezwe kwenye kilimo katika hii Dira mpya ili tuweze kuwa na kilimo cha kisasa kisichotegemea mvua”

Maadhimisho hayo ya Uhuru yamebeba kauli mbiu isemayo “Umoja na mshikamano ni chachu ya maendeleo ya taifa letu” kauli mbiu inayotilia mkazo umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wa taifa hilo katika juhudi za kuleta maendeleo endelevu.

Imeandaliwa na Amri Ramadhani Sauti ya Amerika Dar es Salaam.

Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika Uwanja wa Taifa - Dar es Salaam
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 leo tarehe 09 Desemba, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
Mnatusumbua vichwa vyetuuuuu.....akija rais mwingine anaziacha hizo dira na miomgozo anakuja na ujinga wake anaacha kufuata hizo mnatuchoshaaas
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 leo tarehe 09 Desemba, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Mkuu hakujawahi kuwa na Uhuru wa Tanzania Bara , ni Uhuru wa Tanganyika , Inasikitisha sana ikiwa hata wewe unaingia kwenye upotoshaji huu .

Mnaogopa nini kuitaja Tanganyika , mkiitaja mtafanywaje , na atakayewafanya hivyo ni nani na kwanini ?
 
Uhuru wa Mtanganyika komando ni Mswahili wa Kizimkazi..........Hii nchi tuna unafiki mwingi sana ndiyo maana hatuendelei
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 leo tarehe 09 Desemba, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Uhuru wa Tanganyika Kiongozi Mkuu kutoka taifa lingine Zanzibar.Hii nchi bado inasafari ndefu sana katika suala zima la kujitambua.

Mwl Nyerere katuachia katiba ya ajabu ajabu kiasi kwamba hta wananchi hawajui thamani ya nchi yao.Hakika Mwl Nyerere hastahili utakatifu hata kidogo kauza uhuru kwa taifa la Zanzibar ambao nao kila siku wanauza rasilimali zetu kwa waarabu.
 
Rais wa Tanganyika yupo wapi?
Rais wa Tanganyika mwenye uchungu na anayejali rasilimali na maslahi ya Watanganyika na Tanganyika yupo wapi?

Huyo hapo SSH ni dalali wa kuuza rasilimali za Tanganyika zote chapchap misitu, mbuga, Bandari. Umeme hakuna, maji shida.
 
tubebugi, wacha tuliwe watanganyika.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 leo tarehe 09 Desemba, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Acheni unafiki wa kijinga, hakuna nchi iliyopewa uhuru na mwingereza inayoitwa Tanzania bara, ni Tanganyika
 
Uhuru na kazi, kazi iendelee, uhuru na maendeleo.

SSH2025/2030

Pisha kulee na meno yako ya kuungua(sijamsema wa singida Wala machame kwa kuwa Wana meno ya kuungua), SSH anapita kuelekea 2030
 
Back
Top Bottom