Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Jina la Tanganika asili yake kwa mjibu wa wapelelezi wa kijerumani lilitokea Kigoma Ujiji (nchi ya rutuba) wakimaanisha samaki wakubwa wanaopatikana ziwa hilo kubwa yaani 'Nika au kwa kabila la wakwendi mwambao wa ziwa hilo waliita ziwa lenye dhoruba'. Hata hivyo wapelelezi hao hawakuishia uchunguzi wao hapo waliendelea kutafiti kutoka makabila mengine ya kibantu kuanzia Kigoma hadi Pwani ambako walikutana na mahusiano ya jina Tanganika na Tanganyika. Alichokibaini ni kwamba katika maelezo ya wasifu wa eneo lote kuanzia mwambao wa ziwa Tanganyika, Ziwa Nyanza (Victoria/ziwa sukuma-kasikazini), Msumbiji hadi Pwani ya Mtwara, Bandar Al Salama na Tanga walimaanisha Tanga ni eneo la kupumzika wavuvi na vyombo vyao vya kuvulia samaki baharini na Matanga (chombo hufungwa Tanga ili upepo usaidie kusukuma uelekeo autakao mvuvi), Nyika ikiimanisha kondeni, shambani, maeneo tambarare ya nchi kavu yanayopakana na bahari, ziwa au mto mkubwa.Ila kusema UKWELI aliyekuja na jina Tanganyika MUNGU anamuona!
Au alijua sisi ni wa-Danganyika??
Make naona tunaishi udanganyifu na kudanganywa danganywa tu!
Ikumbukwe kuwa mwanzo Tanganyika ilikuwa koloni la Kijerumani ikijumuisha Tanzania bara ya leo, Burundi, Rwanda, Zanzibar, Kongo na kasikazini mwa Msumbiji hasa jimbo la kasikazini la Cabo Delgado. Hata hivyo baada ya vita ya kwanza ya dunia kuisha waingereza na wabeligiji waligawana maeneo hayo ambapo Kongo, Burundi na Rwanda walichukua wabeligiji huku wakoloni wa Msumbiji (Wareno) wakachukua eneo la kasikazini linalopakana na Tanganyika kwenye mto Ruvuma.
Kwa ujumla Tanganyika ni eneo la wakazi wanaopatikana mwambao wa bahari ya hindi kuanzia mto Ruvuma, Mtwara hadi Tanga, kasikazini kuanzia Kilimanjaro hadi Kagera (zamani ziwa magharibi), madharibi kuanzia Kigoma hadi Rukwa, kusini kuanzia Mbeya hadi Ruvuma wenyeji wanaopatikana maeneo hayo hadi katikati ya nchi ndio inaitwa ''TANGANIKA' au 'TANGANYIKA'
Ikumbukwe kwamba Sultan wa Zanzibar wakati wa enzi wa utumwa alikuwa na mamlaka ya kiutawala maeneo yote yaliyopitiwa na msafara wa watumwa kama Kigoma, Tabora, Manyoni (Singida), Dodoma, Morogoro, Pwani, Lindi, Bandar Al Salama na Tanga