Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mashindano Makubwa ya Qur'aan kwa Wanawake Duniani Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, leo tarehe 31 Agosti, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameshiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Tukio hili muhimu limeakisi dhamira ya Rais Samia ya kuendeleza umoja wa kitaifa na kudumisha amani katika nchi yetu.
Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa haki, amani, kuheshimiana, na kustahimiliana kama nguzo za kuimarisha umoja wetu kama taifa. Ameeleza kuwa mashindano haya yanachangia katika kuimarisha maadili ya kitaifa na kudumisha mshikamano miongoni mwa wananchi wa Tanzania bila kujali tofauti za kidini au kikabila.
Rais Samia pia amegusia umuhimu wa kuendeleza familia zetu na maadili ya nchi, akibainisha kuwa familia yenye misingi imara ni msingi wa taifa lenye nguvu. Amehimiza wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika mazingira ya heshima, amani, na upendo ili kuijenga jamii yenye maadili bora.
Mashindano haya ya Qur'aan yameleta pamoja washiriki kutoka mataifa mbalimbali, yakiwa ni jukwaa muhimu la kukuza maadili, uelewano, na mshikamano wa kimataifa. Rais Samia amewapongeza washiriki wote na kuwatakia kila la heri katika mashindano hayo, akisisitiza kuwa washindi ni wale wote waliohudhuria na kushiriki kwa dhati.
Mwisho, Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kudumisha amani, mshikamano, na maadili mema ili kuhakikisha kuwa Tanzania inabaki kuwa kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa duniani.
#######
Rais Samia Suluhu Hassan,
Amesema unapomlea binti vizuri kidini, akayasoma na kuyaelewa mafunzo ya kidini, ni dhahiri kwamba atakuja kuwa mama bora katika siku za baadaye na kuja kuwa mlezi mzuri wa familia na jamii yake.Kwa maoni yangu Mtoto wa kike akipata elimu ya dini vizuri na sio tu kuisoma Quran lakini aisome na ajue zinasema nini, Mabinti hawa wanapaswa kuendelezwa kwa namna zote, Mwanamke ni Chuo chema ukimuandaa vizuri”
Mashindano haya [kuhifadhi Quran] ni faraja kwa watoto wetu wanaoshiriki na wanaoandaliwa kuwa raia na wazazi wema, kwahiyo ni vema tukaweka nguvu kukuza zaidi mashindano ya aina haya.
Kukubalika kwetu [ulimwenguni] pamoja na rehema za Mwenyezi Mungu, ni kutokana na jitihada zetu za kuendeleza umoja wa kitaifa na kudumisha amani nchini kwetu, hivyo niwasihi Watanzania wenzangu, tuendelee kuilinda heshima hii kwa kudumisha amani nchini kwetu