Rais Samia ashuhudia utiaji saini mikataba ya Mradi wa Maji wa Miji 28 - Chamwino (Dodoma), Juni 6, 2022

Rais Samia ashuhudia utiaji saini mikataba ya Mradi wa Maji wa Miji 28 - Chamwino (Dodoma), Juni 6, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia akishuhudia utiaji saini mikataba ya Mradi wa Maji wa Miji 28 - Chamwino Jijini Dodoma, Juni 6, 2022.



=======
Samia Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Viongozi wote mliopo na wote mliokuja kushuhudia utiaji saini, Jamhuri ya Muungano, Kazi iendelee

Ndugu zangu ni neema nyingine kutoka kwa Mungu na tumshukuru sana kutukutanisha hapa kwa tukio jingine ambalo linakwenda kutatua kero za wananchi. Tunamuomba Mungu azidi kuitunza nchi yetu iendelee kuwa salama na kuwajalia watanzania wote afya njema ili tuweze kuijenga nchi yetu.

Nimpongeze Waziri wa maji na wizara nzima na wafanyakazi wote katika idara ya maji, kwa kazi nzuri wanayofanya kule, shukurani nyingine ziende kwa Waziri wa fedha nilikuwa nikipata mtikisiko kule namwita namuuliza nini shida, tumekwama wapi nataka mkopo huu utoke, na mpaka tumefikia hapa nawapongeza sana.

Tunafanya maendeleo ya nchoi yetu iwe umeme maji nk ila leo tuko hapa kwa ajili ya maji, tunafanya yote haya kwa mfuko wa serikali na wadau binafsi kila jiwe tunaloweza kulipindua tunfanya hivyo ili tuweze kufikia lengo. Na mradi huu tunafanya kupitia wenzetu wa India ambao wametupa mkopo wa Dola milioni 500, na mradi huu ni mkubwa kati ya miradi inayoendelea.

Lakini India wamekuwa wakituunga mkono kutokana na mahusiano yetu, mahusiano ya kibiashara tuliyonayo na wenzetu wametuzidi kidogo ila tukijitahidi kidogo kulima maparachichi tunaweza kwenda sawa, na India wamekuwa wakitupa fursa nyingi za masomo. Nitumie fursa hii kumuomba balozi aweze kuwavuta watu wa India waweze kuja kuwekeza Tanzania.

Wizara ya maji, niwapongeze sana kwa kuwa mmebadilika mno, mmebadilika sana, mlinipa tabu mno mwanzo lakini sasa mmebadilika na mmekuwa vizuri, Mmejitahidi sana kubana matumizi, mradi mmoja unazaa fedha za kwenda kwenye mradi mwingine.

Kuna mradi mwingine ilikuwa ni visima unakuta mabomba yamelazwa ila maji hakuna, au visima vinachimbwa maji hakuna nikamwambia Aweso sitaki huo upuuzi, nedneni mkatekeleze mradi mmoja baada ya mwingine ili maji yapatikane, nendeni mkasimamie miradi vuzuri, kuna tatizo kaeni mzungumze, njoo kwa katibu mkuu mzungumze au njooni kwangu tuzungumze tutatue tatizo.

Nendeni mkasimamie miradi, mkasimamie wakandarasi vizuri, kila mfanyabiashara lengo lake ni kupunguza gharama, usipomsimamia atapunguza gharama na kukuumiza wewe hivyo mkawasimamie wakandarasi ili fedha ikafanye miradi kwa lengo kusudiwa, hiipesa ni mkopo, na kila mtanzania talipa mkopo huu nendeni mkasiamie pesa hiyo, tuliyokopeshwa mabyo ni dola milioni 500.

Nirudie tena shukrani zangu kwa Wizara ya maji lakini pia nihimize ushirikiano kwatika taasisis za serikali, kwani taasisis za serikali zikishirikiana mambo yatakuwa yanakwenda kwa wepesi.
 
Hiz hera nakumbuka jiwe alizifukuzia sana wakawa wanachelewachelewa angalua zimetoka.Ngoja tuone maji yakitufikia sote
 
Back
Top Bottom