Rais Samia asihurumiwe kwakuwa ni mwanamke; kiongozi wa nchi lazima awe na ngozi ngumu. Wapambe acheni kulialia

Rais Samia asihurumiwe kwakuwa ni mwanamke; kiongozi wa nchi lazima awe na ngozi ngumu. Wapambe acheni kulialia

Kauli ya Mdude Nyagali kwenye nchi ya kidemokrasia ni kauli ya kawaida sana.

Kama tulimnyoa jiwe, hata Samia naye alileta udikteta tutamnyoa vilevile
 
Neno "Kunyoa" ni tusi? In fact inategemea umelichukulia katika muktadha upi. Chadema walishakomazwa na kila aina ya uhuni kutoka awamu ya tano hivyo wanajua wanafanya nini. Wanachukua tahadhari kwani hata Magufuli alianza hivi hivi mwisho yaliyotokea kila mmoja wetu ni shahidi.
kunyoa wala si tusi,wala mdude hajawahi kutukana.

maana anacheza vyema na maneno,ambayo ukimpeleka mahakamani humkuti na hatia.

hata mimi nidai hapa jukwaani nimekukaza wewe GSam,ni watu wote wataelewa namaanisha nini,ila mahakama haitelewa.
 
Tatizo kubwa la Watanzania ni kutokujua haki zao na nafasi zao katika Taifa. Itachukua muda mrefu watu kujua haki na wajibu wao kwa Taifa. Kitendo cha kumfanya Rais au kiongozi ye yote kuwa kama mfalme ni kosa kubwa. Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa viongozi wao ni raia sawa na wao na viongozi hawapaswi kupewa hadhi tofauti na wananchi wengine. Viongozi waheshimiwe sawa na raia wengine na siyo kutukuzwa kama miungu watu.

Hivyo kumkosoa kiongozi siyo dhambi ili mradi utu wake haujadhalilishwa, haijalishi ukali wa maneno ya kukosoa. Kitendo cha kuremba remba maneno ya kumkosoa kiongozi kunamfanya ajione ni mtukufu fulani kumbe ni raia sawa na wengine. Kama kiongozi anajiona ana utukufu fulani basi asigombee uongozi abaki na familia yake atukuzwe.

Viongozi wetu siyo wafalme, waheshimiwe kwa umri wao na matendo yao!
 
Moja ya mbinu muhimu kwenye siasa ni kujua nini cha kusema, kwa wakati gani, kwa namna gani na wapi pa kukaa kimya.

Yawezekana kabisa kudai katiba mpya kistaarabu, na uthibitisho upo kwenye mchakato uliopita wa kudai katiba mpya chini ya mwavuli wa UKAWA.

Mna uhuru wa kutumia lugha mbovu lakini athari yake kubwa ni kutengwa na kundi muhimu kwenye siasa za Tanzania: watu wasio na chama. CCM pamoja na mbinu zake chafu hujihangaisha sana ili ikubalike kwenye kundi hilo.

Sasa busara kidogo tu zilipaswa kuwaambia kuwa japo Mama Samia ni Rais lakini pia ni MWANAMKE. Na mkiendelea kujitoa ufahamu, mtongea hoja za msingi lakini Watanzania wengi watawaona kuwa ninyi mnam-bully Mama Samia.

Kujaribu ku-justify lugha isiyo ya kistaarabu ya Mdude kunazidi kuonyesha how hopeless you people are. Lakini sio la kushangaza maana hata yule "mwanaharakati" aliyewahi kumtukana Mwenyekiti wenu na kumuita "jambazi" leo ni swahiba wenu, na mwakalia kimya unyanyasaji anaoufanya dhidi ya watu wasio na hatia. Birds of a feather?

Finally, katiba mpya wanayostahili Watanzania ni ya Watanzania wote na sio ya "Chadema na wanaharakati." Mpo sahihi kuipigania kwa sababu nanyi ni Watanzania lakini msibinafsishe suala hili kuwa lenu peke yenu. Na msitukane pindi mnapokutana na hoja zinazokinzana na hoja zenu.

Baadhi ya wanachama wenu wamemtukana Prof Issa Shivji kwa "kosa" la kutahadharisha kuwa katiba mpya si jambo la kukurupuka. Baadhi yenu mmedai "anazeeka vibaya" huku wengine wakidai anatafuta u-DC. Ieleweke tu kuwa kamwe katiba mpya haitopatikana kwa niia za kihuni
Ujinga uliotamalaki? Mlipoibiwa kura Oktoba mwaka jana na Lissu akawaomba mfanye maandamano, mlitokea? Ndugai na NEC wamelazimisha wabunge 19 mpaka leo, mmefanya nini?

Ni aidha hujui kabisa siasa za CCM wala siasa za upinzani ama huwajui kabisa watanzania wenyewe, ngoja nikusaidie kudogo.

Umeanza kwa kuelezea mbinu za siasa bila Shaka kwa mtazamo wako mwenyewe.

Je, nikuulize swali dogo ni mara ngapi sisi CCM tumejaribu kuzungumza kwenye majukwaa ya kisiasa kwa kutumia mbinu hii? Au mbinu yako uliyotaja wewe inapaswa kutumika kwa wapinzani peke yao?

Naomba nikuambie kuwa kama kuna wa kutumia mbinu hii basi ni sisi CCM kwa sababu Sisi ndio tunaongoza serikali, na mashambulizi yote yanaelekezwa kwetu.

Nikukumbushe pia wapinzani wana uhakika kwa asilimia zote kuwa hata kama katiba mpya itapatikana haitakuwa suluhu za siasa zao Kwa asilimia zote Kwa sababu wanajua fika kuwa wana CCM watateka mchakato mzima na ku drive the way watakavyo wao.

Wanachofanya wapinzani 'strategically' ni kujitahidi kuwa relevant kwenye majukwaa ya kisiasa kila siku Kwa kadri iwezekanavyo. Wakati wewe na wengine mnaona kauli ya Mdude sio ya kistaarabu na kuibua discussions nyingi wao wapinzani wanaona 'mission imefanikiwa'

Pia, as the matter of facts kauli ya Mdude kwenye majukwaa ya kisiasa inaadhari gani hasa kauli ile ikitolewa kwenye majukwaa ya kisiasa? Hv unafahamu vema kauli zilizokuwa zinatolewa na wana CCM tena viongozi kama vile Dunia hii ni ya CCM? Na ndio maana nikasema sidhani kama unafahamu vema hizi siasa za CCM na wapinzani.

Kwa maoni yangu mimi, Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa chama hakupaswa kusema apewe muda Kwa ajili ya Katiba Mpya Kwa sababu kwamba anasimamisha nchi Kwanza. Alichopaswa kusema ni kuwa anaanda utaratibu mzuri wa namna ya kuwaashirikisha wadau mbali mbali ili swala hili lifanyike kwa ufanisi unaostahili. Mwenyekiti wetu alipozungumza siku ile ni kama vile katiba mpya ni 'hisani yake mwenyewe' na hali hii ndio iliochochea vuguvugu kubwa kila mahali.

Rais wetu angesema anaandaa utaratibu mzuri mbona angeweza kunyamaza wala asihangaike na utaratibu hata miaka 5 mbele huko maana hakuna popote anakoweza kubananishwa kuhusu utaratibu zaidi ya maneno ya kisiasa.

Kikubwa nachokiona kwa CCM ni mara Kwa mara wanatoa platform Kwa wapinzani bila wao kujua.

Labda, nikuulize Jambo. Hv kweli wewe unawaona wapinzani walio serious kutawala nchi? As the matter of fact, hawapo, bali kuna kundi la wapiga kelele na kusumbuana tu.

Kama ulivyosema 2019 na 2020 CCM tumezoea viti vyote vya uchaguzi, niambie wapinzani hawa wamefanya kitu gani kuonyesha Yes, they are serious and very determined.

Kwa kumalizia, ndio Mama yetu Rais ni mwanamke lakini nchi haiwezi kukubali treatment ya namna hio kwenye nafasi kubwa ya kitaifa. Kumbuka Mama hajapewa kazi ya kubeba matofali Bali ni kazi ya kutumia akili na utashi na wasaidizi wake Kwa waume wapo.

Sisi kama CCM tunamuona Mama Sawa na ambavyo tungemuona mwanaume kwenye kiti cha Urais. Na kiukweli Mama yetu anatosha
 
Back
Top Bottom