Rais Samia: Asilimia 93 ya Uchumi wa serikali zote duniani ni deni Tanzania inadeni dogo sana ukilinganisha na wenzetu

Rais Samia: Asilimia 93 ya Uchumi wa serikali zote duniani ni deni Tanzania inadeni dogo sana ukilinganisha na wenzetu

Mshindi wa Vita

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2025
Posts
315
Reaction score
139
Akihutubia mkutano wa kampeni, Rais Samia Suluhu Hassan alieleza hali ya deni la Serikali, akisema kuwa hadi kufikia mwaka 2024, deni la Serikali zote duniani lilifikia asilimia 93 ya Pato la Dunia (GDP), huku deni la Serikali za Afrika likiwa asilimia 67. Kwa Ukanda wa Afrika Mashariki (EAC), deni hili lilifikia asilimia 69 ya Pato, wakati Tanzania ikiendelea kuwa na deni la chini zaidi likifikia asilimia 46 ya Pato la Taifa, jambo linaloashiria udhibiti wa kifedha unaowawezesha kuendeleza miradi ya maendeleo bila vikwazo vikubwa vya kifedha.
 
sio kweli
Kinachonifurahisha wanaoambiwa takwimu kwa asilimia hakuna hata mmoja anajua maana ya kinachozungumzwa huwa mnabubujikwa mahaba ya elfu kumi kumi mlizopewa mkashangalie mkisharudi mtaani kwenye uhalisia wa maisha ndiyo akili zinawafunguka huku mmepauka balaa.

Kama hapa,umeng’ang’ana ”siyo kweli ni kweli” wewe ulitegemea apande jukwaani awaambie ukweli deni la taifa ni kubwa halilipiki?
 
Kuna hasara gani ya kutokuwa na deni na Kuna faida gani ya kuwa na deni??? Tukipata jibu hapa mambo yote yatakuwa mseleleko!
 
Back
Top Bottom