Rais Samia: Jingine ni lile la asilimia kumi, Dodoma wamesema vizuri hapa, hongera mstahiki meya na mkuu wa mkoa. Wamesema vizuri kwamba wanajipanga sasa kwa ajili ya kutoa visenti vichache kwa kila kundi na mimi huwa nasema, fungu lile lilikuwa linatumika kama mfuko wa kisiasa wa madiwani, kila diwani anapeleka kwake vijipesapesa kujipendekeza kwa watu ili ateuliwe lakini huoni kilichofanyika.
Sasa watu wajipange kutoa fedha kwa vikundi vikubwa vyenye miradi mikubwa ambayo impact yake itaonekana, mnatoa milioni 40 kwa kikundi kwa mfano, milioni 100 kwa kikundi lakini mna hakika zitaenda kufanya mradi utakaowapa wao ajira, utaowaajiri wenzao na faida zinaonekana.
Sio kugawa kidogo kidogo kujipendekeza kwa wapiga kura ili uje kupigiwa kura na mfuko huu tunaua kwa maslahi binafsi.