Rais Samia atakuwepo madarakani hadi 2035?

narudi kesho

Senior Member
Joined
Jul 5, 2024
Posts
177
Reaction score
270
Hili swali kidogo linanitatiza. Je, Rais mama yetu Dkt. Samia atakuwepo hadi 2035? Nauliza hivyo maana utaratibu wetu wa kuongoza nchi ni 10 years.

Sasa hapa Rais wetu atakuwa ameongoza kwa 14 years. Kwa kule USA Trump ameambiwa hatakama atashinda uchaguzi ila ata ongoza kwa muhula 1 ambao ni 4 years.

Hapo kwetu ipoje mi naona akiongoza hadi 2030 na uchaguzi wa Rais mwakani usifanyike ila chaguzi zengine zifanyike. Hayo ni maoni yangu unaruhusiwa kunikosoa.

Mnaoelewa hili zaidi nahitaji muongozo wenu.
 
Kuna IDs mpya zinakuja na hii suggestion Kila mara mnaspin nini!!?

Kama uhakika upo kwanini kuuliza uliza was ids mpya!!?mnataka kumfanyaje mhusika kama Kila kitu in place!!?

Na mimi nauliza tu!!

Hasta jpm ilikua hivihivi eti Bunge la vipindi saba!!

CCM tumeamua kuwa ni yeye 2025,sasa mbona spinning!!?
 
Nyie endeleeni tu kumchuria huyo mama yenu. Yeye mwenyewe alishasema hataki tena.
 

Attachments

  • 5744975-8bcb85f1807b40dfe9b1bdf5a6eabbb0.jpg
    8 KB · Views: 3
Dah! Wewe ni member mpya kweli?

Umejiunga ijumaa hata wiki huna.

Halafu unasema eti narudi kesho

Hata usiporudi ni sawa tu maana una id nyingine tayari.
 
Jamani hii huru anaruhusiwa mtu yeyote kuuliza
 
Katiba inakifungu kuwa awamu itahesabika kuwa haijatimia ikiwa tu aliyekaimu kaongeza kwa less than 3 years, yeye hii awamu kaongoza kwa more than 4 years so anaruhusiwa kuongoza tena miaka 5 unless wabadili vifungu au wapuuzie katiba kama kawaida yao.
 
Sawa ahsante kwa majibu mazuri maana member wengine wanalaumu tu.
 
Tukichukulia muhula wake rasmi uanze mwakani 2025, baada ya kumaliza kumshikia Joni, halafu hiyo miaka 7 ipitishwe Bungeni, basi tutakuwa naye hadi 2040 hapo!

2025 + 7 + 7 = 2039

Kwa hiyo tukaeni mkao wa biriani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…