The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Katika watu ambao historia ya Tanzania huwa haiwatendei haki basi Rashid Mfaume Kawawa anaongoza - ni nadra Sana kusikia historia sahihi ya Kawawa.
Mara nyingi Historia yote ya Nyerere inaweza somwa na usisikie hata jina la Kawawa. Watu wengi hawajui kuwa wakati Kawawa anakuwa 'Waziri Mkuu wa Tanganyika' alikuwa Kiongozi mkubwa kuliko wote Tanganyika kabla haijawa Jamhuri..
Kawawa alikuwa Waziri Mkuu baada ya Nyerere kijiuzulu..mpaka Leo hiko kipande cha historia hakieleweki vizuri.. Itoshe kusema kama Kawawa angekuwa na tamaa ya Uongozi kama Viongozi wengine Africa basi Nyerere hata huo urais angekuja kuusikia kwenye bomba.
Nyerere alijiuzulu Uwaziri Mkuu wa Tanganyika na kumkabidhi madaraka Kawawa halafu ilipofika tarehe 9December 1962 Nyerere akarudi kuja kuapa kuwa Rais wa kwanza Tanganyika. Kawawa akiwezesha zoezi lote hilo.
Ndo maana siku Ile Kambona alipokuja kuwashambulia Kawawa, Nyerere na Amir Jamal. Nyerere alisema anaweza kukaa kimyaa akishambuliwa yeye lakini hawezi kunyamaza watu wakimshambulia Kawawa...akasema kama Kawawa sio muaminifu basi hakuna watu waaminifu duniani.
Hata siku anastaafu Nyerere aliongea huku machozi yanamtoka akisema 'Kawawa nakushukuru sana'. Ulibeba lawama zangu zote zikawa zako.
Hakuna kiongozi aliyewahi kubeba lawama za Rais Tanzania kama Kawawa... Zoezi la Vijiji vya ujamaa lilipoleta njaa na vifo ..Kawawa alibeba lawama peke yake.
Kawawa alikuwa muaminifu na mtiifu kwa Nyerere haijawahi tokea.....aliziba udhaifu wa Rais na kumlinda na lawama za kila aina..
Sio kila Rais wa Tanzania anapata bahati ya kuwa na msaidizi kama Kawawa ..Mwinyi alipata Waziri Mkuu Malecela alietamani kuwa Rais akijiandaa na kushindana na wanaotaka urais wengine. Hakukubali kuchafuka kwa niaba ya Rais.
Mkapa alipata Sumaye ambae alikuwa kila kitu ni kama hawezi hadi wakampachika jina la Zero.
Kikwete akamchagua Rafiki yake Lowassa..wakawa kama 'marais wawili'.
Kama kuna kitu Rais Samia anahitaji sasa ni Kumpata 'Rashid Kawawa’ wa kwake.
Lakini je atampata wapi?
Tunao Viongozi watiifu na waaminifu wa kumlinda na kumsaidia Rais na kukubali kubeba lawama zote na kuchafuka kwa niaba ya Rais? Walk wapi?