Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anazindua nembo na tarehe ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, leo tarehe 08 Aprili, 2022 Golden Tulip Hotel, Zanzibar.
Rais Samia ameanza kuzungumza muda huu...
Rais Samia: "Taarifa nilizonazo ni kuwa oparesheni inaendelea vizuri, Watanzania wanashiriki kikamilifu, nawashukuru kwa uzalendo."
Ametangaza kuwa Agosti 23, 2022 kuwa tarehe rasmi ya sensa nchini.
"Haitapendeza kusikia kuna watu wamekataa kuhesabiwa.
"Kwa muda uliosalia hadi kufikia Agosti mwaka huu ni muda mfupi, lakini kazi zote za msingi kuhusu sensa zimekamilika, zilizobaki ni kazi za kiufundi.
"Sensa sio jambo geni kufanyika katika nchi yetu, zimeshafanyika sensa tano tangu tupate uhuru, zimefanyika katika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002, 20212 na sasa 2022.
"Kila Mtanzania aliye hai ahesabiwe, ili tukijipanga tujue tunajipanga kwa namna gani. Serikali haiwezi kupanga mipango ya maendeleo bila kuwa na takwimu sahihi.
"Ni jambo la faraja kwa nchi yetu, kwa kupeperusha bendera yetu ya sensa katika Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia idadi ya watu mwaka huu.
"Nembo hii ninayoizindua leo itumike na idara zote, kwa taasisi ambazo zitakuwa na vipindi TV, nembo hii itumike kote, pia mnaweza kuweka kwenye tiketi.
"Napenda kutamka wazi kuwa tarehe 23 Agosti mwaka 2022 ndiyo siku maalum ya sensa ya watu na makazi," Rais Samia.
===========================
Sensa 2022 kufanyika siku ya kazi kukwepa siku ya ibada
Kuelekea kufanyika kwa zoezi la sensa mwaka huu Serikali imesema imesikia kilio cha viongozi wa ibada kutofanyika siku ya ibara, hivyo itafanyika siku za kazi ili kukwepa suala la ibada kwa waumini wa dini mbalimbali
Akizungumza wakati wa uinduzi wa Nembo na Tarehe ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema: “Hadi kufikia Machi 31, 2022 maandalizi ya sensa yamefikia kwa asilimia 79.
“Kwa kuwa sensa inafanyika kila baada ya miaka 10, zoezi la sasa litatumika kama rejea kwa miaka 10 ijayo, ndiyo maana tumeshirikisha wadau na litafanyika kwa umakini mkubwa.”