Rais Samia atangaza siku 5 za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth aliyekuwa Mkuu wa Nchi ya Tanganyika

Alikuwa mkuu wa Tanganyika kwa mwaka mmoja na alisaini hati za uhuru.

Kwa mustakabali wa diplomasia ni jambo jema kufanya hili.

Haya tuungane.
lakn diplomasia hio hio inasema akifa wa kwetu wasiweke nusu mlingoti? Alipokuja kukukalieni kichwani mlifanya makubaliano kuwa awakalie?
 
jumuiya ya madola ni muendlezo wa ukoloni kwa lugha tamu...
 
Kwani na wao wanazileta bure.......timing tu ,tunakula walivyotuibia
Duniani hakuna cha bure, zaidi ya salamu tu,
Uk wanaongoza kwa uwekezaji hapa Tz, unajua wananufaika kwa kiasi gani,

kutokana na mikataba ya ovyo walioingia watawala wetu?
 
Zilipotea Mkuu mambo ya UTAWALA BORA

Two years back...niliiipata ila kwa mbinde sana Mkuu kupitia hukohuko kwao SKOTISHI tena kwa heshima ya Julius upande wa Conservation
hata mwaka huu zilikuwepo mi nilikuta deadline tyari ilikuwa june
 
Nashauri ndege zetu zitupeleke msibani UK, tukamlilie malkia Liz,
siku tano kukaa uzunguni tuapunguza machungu ya tozo,
Tukirudi watuache Bujumbura Burundi kwa kutii agizo la Nchemba Madilu,
Unajua kabisaaa kuwa tunaomboleza na hakika macho yamevimba kwa kumilia Lizabeta.
 
Aliyewatawala akawapeleka utumwani, akawauza kama nyanya, akawafanyia madhila yasio ya kibinadamu. Bado tuna safari ndefu kama wafrika. Itoshe kusema pole inatosha na sio zaidi.
 
Na hiyo so called Commonwealth inatusaidia nini haswa? Alivyokufa Baba wa Taifa waliomboleza siku ngapi? Siku moja nusu mlingoti ingetosha kabisa! Utumwa wa akili! Ukoloni mamboleo!
 
Kwa wanaopinga binafsi mimi sioni kama hili ni Big Deal (Sisi pia tupo kwenye Commonwealth), hilo ni moja pili kupepea bendera nusu mlingoti haitupunguzii kitu wala haituongezei Tozo..., ila its a good gesture kwa kesho na keshokutwa ambayo huenda ika-pay off....

We should always try to build bridges even with our enemies...,
 
Na hiyo so called Commonwealth inatusaidia nini haswa? Alivyokufa Baba wa Taifa waliomboleza siku ngapi? Siku moja nusu mlingoti ingetosha kabisa! Utumwa wa akili! Ukoloni mamboleo!
Hujuia chochote Kaa kimyaa
 
70% ya bidhaa zetu tulikuwa tuna import wakati huo kutokana na kuwa Taifa letu lilikuwa changa bado na viwanda ndio kwanza Mwl alikuwa anaanza kuvijenga, hivyo kuficha aibu ya babu zetu kutokana umaskini wa wakati huo, uingereza walifanya jitihada za kila namna ili tuishi kama civilized people.

Tuliletewa nguo, mashine mbalimbali, vifaa vya nyumbani kama vile radio za phillips, majiko ya umeme, Ukumbuke wakati huo hakuna umeme maeneo mengi, hivyo kuishi kwenye nyumba ya umeme, maji na simu, ilikuwa kwa watu wachache. (the privileged) Kuwafikia watu ili wapate habari ilibidi kununua redio za betri (koroboi) na wakati huo kituo cha redio RTD ndio kiliaanzishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…