70% ya bidhaa zetu tulikuwa tuna import wakati huo kutokana na kuwa Taifa letu lilikuwa changa bado na viwanda ndio kwanza Mwl alikuwa anaanza kuvijenga, hivyo kuficha aibu ya babu zetu kutokana umaskini wa wakati huo, uingereza walifanya jitihada za kila namna ili tuishi kama civilized people.
Tuliletewa nguo, mashine mbalimbali, vifaa vya nyumbani kama vile radio za phillips, majiko ya umeme, Ukumbuke wakati huo hakuna umeme maeneo mengi, hivyo kuishi kwenye nyumba ya umeme, maji na simu, ilikuwa kwa watu wachache. (the privileged) Kuwafikia watu ili wapate habari ilibidi kununua redio za betri (koroboi) na wakati huo kituo cha redio RTD ndio kiliaanzishwa.