Rais Samia atangaza siku 5 za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth aliyekuwa Mkuu wa Nchi ya Tanganyika

Mwana JF aliyemkumbusha Rais Samia kupeperusha bendera nusu mlingoti amemuokoa Rais asidukuliwe moyo.
 
Alikuwa mkuu wa Tanganyika kwa mwaka mmoja na alisaini hati za uhuru.

Kwa mustakabali wa diplomasia ni jambo jema kufanya hili.

Haya tuungane.
Kama ndivyo kwanini na sisi tukipata majanga ya vifo wao hawafanyi lolote? Huu unyonge tu wakujitakia, basi...Diplomacy ya one side ina umaana gani na thamani gani kwetu?
 
Kama ndivyo yenyewe U.K ambapo alikuwepo huyo mtawala hatambui nchi za jumuiya yake wanapopatwa na vifo? Diplomacy ya kukandamiza wengine huku wao wakijitukuza inafaida gani kwenye century hii ya leo? Watanzania tuache huu unyonge, mental slavery ni mbaya sana kuliko ule ukoloni halisi wa mijeledi
 
Ni suala jema kwa ustawi wa dipmalomasia ya Tanzania na nchi za Commonwealth na dunia.
 
Huyu ni mwasisi wa nchi ya Tanganyika hivyo heshima zote anastahili kupewa.
 
Hongera Mheshimiwa rais kwa uzalendo uliotukuka
 
Hata India wameshusha sasa sisi tunashangaa nini?
 
Hao ni vijana wa Magufuri ambao wanajifanya wana elimu kubwa,hata historia ya nchi hawaijui.
 
vizuri sana Rais Samia anaendeleza kuimalisha diplomasia
 
Mazishi yanategemewa kuwa 19/9/22.
 
Siku 5 ni muafaka tukizingatia ukweli wa Kihistoria alikuwa ndiye mkuu wa nchi ya Tanganyika huru wa kwanza tena mwanamke. Tanganyika huru kama na utaratibu huu ungaliendelea kwa sasa tungekuwa na Malkia 11 kututawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…