kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga wamemsifu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uamuzi wake wa kusitisha utaratibu uliotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwataka kuanza kutumia mashine za kieletroniki (EFD) katika kufanya malipo.
Sambamba na hilo wamemwomba Rais Dkt. Samia kuunda kikosi kazi kitachojumuisha viongozi wa wamachinga nchini, TRA, Jeshi la Polisi, Viongozi kutoka Halmashauri pamoja na wawakilishi wa serikali, kukaa na kufanya upembuzi wa kuwatambua wamachinga halisi ili kuzuia wafanyabiashara wasiokua na sifa ya kuwa machinga kujipenyeza kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.
Nae Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alitoa ufafanuzi juu ya suala hili alipoulizwa na kituo kimoja cha Runinga na kusema
"Nitoe rai Machinga wasipate taharuki yoyote na Rais amelishalitolea ufafanuzi na mantiki ilikuwa sio Machinga ilikuwa ni maeneo mahsusi ya matumizi ya EFD lakini ilivyotafsiriwa ni machinga pekee lakini zoezi halijalenga hivyo, lililenga maeneo mahsusi ambayo ya matumizi ya EFD"- Waziri Mwigulu Nchemba