Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Taasisi zote za ulinzi na usalama zipo hapo bandarini.
Tatizo la msingi ni maadili ya "rasilimali watu" wanaopewa kutekeleza majukumu yao pale.
Kijana wa "teeth" (tamka tiithi) anapelekwa pale akiwa na ndoto za kumiliki jumba la kifahari pale Mbweni na Toyota Prado TX.
Takukuru vivyo hivyo.
Polisi nao ni vivyo hivyo.
Wavaa mabaka nao vivyo hivyo.
Kuli naye vivyo hivyo.
Dereva naye vivyo hivyo.
Afisa forodha naye vivyo hivyo.
Bodi, Kamati ya Bunge,RC, RPC, RSO, DC, OCD, DSO.
Kwa mnyororo huo,kweli tunategemea bandarini pawe salama!!??
Pale Nyamisati pana bandari inapitisha mamia ya tani za mizigo kila leo,na mamlaka husika wanajua,lakini hakuna hatua zinachukuliwa.
 
Bandari haitaji miguvu
Mzee inahitaji akili,ubunifu
Weledi,mtendaji
Hao wajeda si walipelekwa kwenye korosho,ilikuwaje

Ova
 
Tanzania mtu akishawekwa kwenye taasisi basi mawazo yake ni kula tu

Ova
 
Ikibinafsishwa ndio inakufa kabisa. Rejea kilichowahi kutokea kwenye Reli, Shirika la ndege na viwanda
Inategemea na vile unavyobinafsisha,wao serikali wanatakiwa kubaki kwenye kusimamia kodi tu,shughuli za kutoa mizigo sekta binafsi wapewe wafanye
 
Kubadilisha mfumu wa uendeshaji ka kanuni. Kwa mfano (siyo lazima iwe hivyo) watu wanaajiriwa kwa mikataba inayozingatia utendaji wao baada ya kushindanishwa na kuchujwa kwa umakini.
Taasisi nyingi wanaajiriwa kwa kushindanishwa mbona napo bado pako hoi?
 
Wazo zuri Ila Nina wasiwasi na huo uthubutu wa kuwapeleka vijana wakajifunze kama utafanyiwa kazi.
 
Bandari haitaji miguvu
Mzee inahitaji akili,ubunifu
Weledi,mtendaji
Hao wajeda si walipelekwa kwenye korosho,ilikuwaje

Ova
inahitaji weledi wa kula mapato?!
inahitaji akili ya kula rushwa?!
hao tunao waita weledi ndio wametufikisha hapo.

Bandarini panahitaji minguvu na weledi vyote kwa pamoja. kuna mifisi maji pale haisikiii wala haiambiliki matokeao yake tunapata hasara kama taifa.

Vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama vimeshindwa kabisa kuidhibiti upotevu wa mapato hapo bandarini?! vimeshindwa kusimamia ufanisi wa bandari??!

ni watu wa aina gani wanao toa huduma ktk bandari zetu haswa bandari ya DSM?!

Kama bandari ya DSM tu ambayo ipo pua na mdomo sasa vipi kuhusu bandari ya KIGOMA? N.K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…