Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Siasa za pale Bandarini ngumu sana

Hakuna cha siasa wala ugumu sema hawajapata mtu sahihi coz pale wanateuliwa kupiga deal na kurudisha marejesho kwa waliowateua. Kazi kama hizo isingekuwa za kuteuana, ingekuwa competence based
 
Matatizo hayako bandarini peke yake.

Matatizo yapo kila mahala, hata kwa wateuzi wenyewe.

Sasa jiulize, hapa katoa usuluhishi gani juu ya tatizo lililopo bandarini.

Huyu bwana mdogo aliyeteuliwa naye siku chache zijazo utasikia kishashindwa kazi.

Mbaya zaidi ni kutochukua muda kufahamu tatizo la sehemu hiyo hasa ni lipi, linalofanya pawe na 'turnover' kubwa kiasi hiki?
Kwa nini watu hawaoni hili?
 
sidhani hata kama hii historia uliyoiweka hapa kuna watu kizazi hiki wanaifahamu, mimi nikiwa mmojawapo

Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania Railways Corporation SGR , Watendaji husika serikali yote, Amos Makala na Shirika la Masoko Kariakoo, naibu spika Zungu na wazee wenzie wa club ya Saigon Kariakoo n.k wanatakiwa wapitie hapa JF wapate elimu isiyofundishwa ktk vyuo vyetu.

Mfano kuvutia itumike basi nchi za Zambia, Malawi, DR Congo, Rwanda, Burundi zipewe ma-gati ya mkataba aina ya BelBases sisi tufanye miaka 99 na upanuzi wa bandari ukifanyika iwe ya DSM au Mtwara pia tuwahusishe majirani watie mkono wao ktk ujenzi wa gati exclusives na pia haki za kutumia reli na pia uwekezaji ktk njia ya reli. Sisi tutaingiza mapato meli ikiingia, pilot wa TPA atatoza ushuru, meli zitanunua, mafuta, maji na chakula cha mabaharia n.k yaani mambo ni mengi ya kuichangamsha bandari ya DSM iwe hub / kitovu cha biashara, Kariakoo itakuwa soko kuu la nchi hizo tajwa n.k sijui mungu huyu atupatie nini ikiwa kina Sultan Seyyid Said na wazungu wa Ubelgiji na Uingereza kupitia BelBases convention German East Africa lakini sisi hatukioni !

Na sisi kizazi cha dot.com intaneti ina siri zote zimewekwa, mbali ya masuala yetu ya ushabiki wa mpira, singeli, amapiano, mwanasiasa kasema nini, celebrity wa kibogo leo ana event au scandal gani, dini ipi bora n.k basi tujitanulie uwingo na kuongeza mengine mengi yawe ya social, elimu, historia, biashara n.k
 
Mi nahisi hivyo. Mabandari, madini, mahifadhi hayajawahi kuwa na faida kwa Raia wa tanzania.
Ndio ukweli wenyewe. Sidhani kama raia wa Tanzania ni nchi hii. Itakuwa pengine ni wakimbizi kutoka kwingineko. Maana! Rwanda, maybe?
 
Binafsisha hizi BANDARI, naona zinatupa shida kubwa kuziendesha au recruits freshers kutoka University, peleka wachache pale Durban, Capetown, Rotterdam, Botswana (dry port)wakajifunze kwa 24mth kuhusu uendeshaji wa hizi bandari, na ajira mpya zifanyike yaani we need to start upya
Hata ulete malaika hizo Bandari ni kichaka Cha wakubwa kupitisha Dili zao na CCM ni Mojawapo kama wangekuwa hawataki hiyo michezo hakuna anayeweza kushindwa kuingiza na kuendesha bandari
 
Matatizo hayako bandarini peke yake.

Matatizo yapo kila mahala, hata kwa wateuzi wenyewe.

Sasa jiulize, hapa katoa usuluhishi gani juu ya tatizo lililopo bandarini.

Huyu bwana mdogo aliyeteuliwa naye siku chache zijazo utasikia kishashindwa kazi.

Mbaya zaidi ni kutochukua muda kufahamu tatizo la sehemu hiyo hasa ni lipi, linalofanya pawe na 'turnover' kubwa kiasi hiki?
Na shida inaonekana kuna watu wanawekwa pale kulinda maslahi fulani hivi? Hatuelezwi kila mara tatizo hasa Nini?
 
Kwa nini watu hawaoni hili?
Pengine ni kwa kuwa hawahojiwi na yeyote katika maamuzi yao.

Wao wakiamua kutumbua, hakuna mtu atakayehoji uamzi huo; na hata sababu za utumbuaji hawalazimiki kuzieleza.

Na kwa bahati mbaya sana, hata mtumbuliwa hana 'recourse' yoyote anayoweza kuiangukia kumsikiliza.

Rais anavyombo vinavyompa taarifa juu ya maswala mbalimbali. Haijulikani kama rais huyo huyo anayo njia nyingine ya ku'verify' aliyo ambiwa na vyombo vyake. Na haijulikani kama huko kwenye vyombo nako wanatumbuana kiasi tunachoona huku kwingine.

Mahali penye tatizo kama bandarini, rais anatakiwa ajiridhishe sana, na ajue taratibu zinazotumika huko na sababu zinazoambatana na hali hiyo, ili aweze kufahamu utatuzi sahihi wa matatizo.
 
Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania Railways Corporation SGR , Watendaji husika serikali yote, Amos Makala na Shirika la Masoko Kariakoo, naibu spika Zungu na wazee wenzie wa club ya Saigon Kariakoo n.k wanatakiwa wapitie hapa JF wapate elimu isiyofundishwa ktk vyuo vyetu.

Mfano kuvutia itumike basi nchi za Zambia, Malawi, DR Congo, Rwanda, Burundi zipewe ma-gati ya mkataba aina ya BelBases sisi tufanye miaka 99 na upanuzi wa bandari ukifanyika iwe ya DSM au Mtwara pia tuwahusishe majirani watie mkono wao ktk ujenzi wa gati exclusives na pia haki za kutumia reli na pia uwekezaji ktk njia ya reli. Sisi tutaingiza mapato meli ikiingia, pilot wa TPA atatoza ushuru, meli zitanunua, mafuta, maji na chakula cha mabaharia n.k yaani mambo ni mengi ya kuichangamsha bandari ya DSM iwe hub / kitovu cha biashara, Kariakoo itakuwa soko kuu la nchi hizo tajwa n.k sijui mungu huyu atupatie nini ikiwa kina Sultan Seyyid Said na wazungu wa Ubelgiji na Uingereza kupitia BelBases convention German East Africa lakini sisi hatukioni !
Mkuu 'Bagamoyo', nimeisoma hii na kujikuta nikijiuliza maswali mengi.

Je, kuna nchi yoyote iliyokwishafanya haya unayoyaeleza hapa na majirani zake, na yakafanikiwa?

Je, umejaribu kuhoji matatizo yanayoweza kutokana na mpango wa namna hii?
Kwa haraka haraka ninaweza kukupa mfano hai kabisa wa kutofaulu kwa mpango huo unaoueleza. Zambia na sisi tunayo pale ile reli aliyotujengea mchina, TAZARA. We huoni matatizo kama hayoyakijitokeza na hao washirika wetu wengine?
Tukianzisha vita na mmoja au zaidi kati yetu na hao washirika kwa sababu mbalimbali, sijui itakuwaje?

Binafsi, nadhani tusitafute kuvumbua dawa mpya kwa magonjwa ambayo yanajulikana na dawa zipo tayari za kuyatibu.
Bandari chungu nzima duniani zinafanya kazi vizuri tu, hizi za huku kwetu tatizo ni nini zisiweze kufanikiwa kama hizo nyinginezo duniani?

Tuache kuhamisha magoli kila mara tunaposhindwa kwa uzembe wetu wenyewe.
 
Je, umejaribu kuhoji matatizo yanayoweza kutokana na mpango wa namna hii?
Kwa haraka haraka ninaweza kukupa mfano hai kabisa wa kutofaulu kwa mpango huo unaoueleza. Zambia na sisi tunayo pale ile reli aliyotujengea mchina, TAZARA.

Tanzania ingejiongeza na kuwapatia Zambia gati mbili huru exclusive bandarini na unafuu wa makodi kama mkataba wa BalBases naamini mpaka leo Zambia wangekuwa wamepewa fursa ya kujenga gati pale TPA DSM port ikawa kama vile ni bandari kavu ya Kapiri Mposhi Zambia ingeendelea kutumia TAZARA, barabara ya TANZAM Highway bila ya kuangalia bandari ya Beira Mozambique wala Durban kule Republic of South Africa.

Na mikataba hii tungekuwa tunaisaini huko MIGA Breach of Contract | Multilateral Investment Guarantee Agency | World Bank Group au Switzerland Investment-Related Dispute Settlement: Towards an inclusive multilateral approach ikizibana serikali za Tanzania au Zambia hata akitokea kiongozi wa kisiasa mwendawazimu asiweze kuichezea.

Lakini nikisome historia ya kwanini TAZARA reli ya uhuru ilijengwa halafu wazee wetu wakashindwa kuona kuwa ipo siku South Africa itafuta ubaguzi, Mozambique nayo ikapata uhuru je Zambia ikitongozwa kupitisha mizigo huko South Africa isiyo ya kibaguzi sisi huku tumeweka chambo gani cha kuifanya Zambia isigeukie huko ? Jibu ni rahisi ni mikakati iliyoona mbali sana isiyotegemea tu maono ya kiongozi mmoja au chama kilichopo madarakani kunahitajika watu wabobevu waona mbali zaidi ya kuwemo ofisini na kila siku kuisoma dunia inaenda vipi kupitia strategy studies na geopolitical situations tuwe hatua mia mbili mbele ya washindani wetu.

Mamikataba ya aina hii inahitaji rasilimali watu wafundishwe wafikie kaliba ya the Tundus Lissus' tofauti na ya kina The Kabudis' ambao hawajui jinsi mikataba na treaties zinaweza kusaidia kuchochea biashara badala ya kuvimbiana sovereignty sovereignty.
 
itafuta ubaguzi, Mozambique nayo ikapata uhuru je Zambia ikitongozwa kupitisha mizigo huko South Africa isiyo ya kibaguzi sisi huku tumeweka chambo gani
Kwa nini usilaumu uwezo wetu wa "kutongoza" ili tuwashinde hao Musumbiji na S. Africa.

Mkuu, 'theory' yako hii ni ngumu kuitekeleza. Sijui kama ulichotaja hapo juu
wa BalBases
ndiyo mfano wa mipango ya namna hii?

SAWA, ni vizuri, palipo na tatizo kuwaza nje ya boksi, lakini hii yako hainipi matumaini.

Lakini nisikukatishe tamaa, jaribu kuijengea hoja, labda kuna siku wataalam wa maeneo haya wataidaka na kuiboresha zaidi; halafu huo ndio unakuwa mwanzo wa "The Bagamoyo Doctrine in Harbour Management."

Nakutakia mafanikio. Siku ikifaulu, usikose kunistua nami nishangilie!
 
Mkuu, 'theory' yako hii ni ngumu kuitekeleza. Sijui kama ulichotaja hapo juu
1657056554946.png

Ni rahisi sana nimeleta mfano huu wa BelBases ambayo umefanyika eneo letu na kitovu chake bandari ya Kigoma na Dar es Salaam ikijumuisha reli ya kati.

Mifano mingine iliyo mbali na Tanzania ipo na inafanya kazi bila wasiwasi. Ambapo Tanzania inaweza kutia saini na mataifa jirani ya Burundi, Rwanda, DR Congo, Zambia na Malawi bila kufanana na huu hapa wa Turkey na jirani zake wakugawa ardhi ya nchi bali Tanzania kutoa haki ya kutumia mfano gati ktk bandari kwa miaka 99 n.k n.k

Treaty of Lausanne, signed in 1923, Eastern Anatolia became part of modern-day Turkey, in exchange for Turkey's relinquishing Ottoman-era claims to the oil-rich Arab lands. Negotiations were undertaken during the Conference of Lausanne. İsmet İnönü was the chief negotiator for Turkey
 
Reli na atc zilishindwa sababu walipewa wasio na sifa na uzoefu.

Bandari kukiwa na ubia na kampuni kubwa Duniani serikali ikashika 51% ,faida itaonekana.
Kuna Dubai port , Nagoya port , busan port , Rotterdam port na Hamburg port

Daressalaam Imekaa sehemu nzuri Katika Afrika , uwekezaji wowote utalipa.

Utendaji wa sasa bado uwezo wake ni mdogo , huyo mkurugenzi aliletwa afanye mabadiliko ameshindwa.
Au ikishindikana waingie ubia wa ushauri wa kitaalamu wa uendeshaji kama walivyofanya Trc wameingia ubia na korail wa uendeshaji na ushauri
Una kichaa wewe sasa hao TRC Wana nini wanafanya kama sio upuuz tu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania Railways Corporation SGR , Watendaji husika serikali yote, Amos Makala na Shirika la Masoko Kariakoo, naibu spika Zungu na wazee wenzie wa club ya Saigon Kariakoo n.k wanatakiwa wapitie hapa JF

06.07.2022
Naibu spika Zungu memba wa Saigon Club kariakoo aongea sakata la TPA


Zungu azungumzia ushushaji mizigo Bandarini



Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amezungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, akisema Serikali imepambana kuondoa usumbufu ikiwemo ucheleweshaji wa ushushaji mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema hapo awali kulikuwa na tatizo la ucheleweshaji mizigo, lakini kwa sasa Serikali imelipatia ufumbuzi na kuwataka wafanyabiashara kuendelea kufanya kazi zao kwa utulivu na kulipa kodi stahiki za Serikali. Pia, amesema kuwa kila mfanyabiashara ana wajibu wa kulipa kodi na kwamba, isitokee mtu amebambikiziwa kodi ama kuonewa isivyo halali. Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, amekutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara na wananchi wakati wa ziara yake kukagua maendeleo na kuzungumza na wapiga kura wake.
Source : mwananchi digital
 
Mdau achambua tatizo la TPA Mamlaka ya Bandari Tanzania



Source: CLOUDSMEDIA
 
Back
Top Bottom