Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania Railways Corporation SGR , Watendaji husika serikali yote, Amos Makala na Shirika la Masoko Kariakoo, naibu spika Zungu na wazee wenzie wa club ya Saigon Kariakoo n.k wanatakiwa wapitie hapa JF wapate elimu isiyofundishwa ktk vyuo vyetu.
Mfano kuvutia itumike basi nchi za Zambia, Malawi, DR Congo, Rwanda, Burundi zipewe ma-gati ya mkataba aina ya BelBases sisi tufanye miaka 99 na upanuzi wa bandari ukifanyika iwe ya DSM au Mtwara pia tuwahusishe majirani watie mkono wao ktk ujenzi wa gati exclusives na pia haki za kutumia reli na pia uwekezaji ktk njia ya reli. Sisi tutaingiza mapato meli ikiingia, pilot wa TPA atatoza ushuru, meli zitanunua, mafuta, maji na chakula cha mabaharia n.k yaani mambo ni mengi ya kuichangamsha bandari ya DSM iwe hub / kitovu cha biashara, Kariakoo itakuwa soko kuu la nchi hizo tajwa n.k sijui mungu huyu atupatie nini ikiwa kina Sultan Seyyid Said na wazungu wa Ubelgiji na Uingereza kupitia BelBases convention German East Africa lakini sisi hatukioni !