Mama'ke Yesu ndiye alitusilimisha, sijamuona bila hijabu.
1 Wakorintho 11:6 BHN
Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
BHN: Biblia Habari Njema
Unaokoteza vifungu vichache vya biblia bila ya kuelewa mantiki na mazingira yake.
Hiyo ni barua ya Mtume Paulo kwa Wakorinto walioomba mwongozo toka kwa Paulo juu ya kufunika kichwa uiongiapo hekaluni.
Na Paulo aliwajibu kwa kadiri ya mapokeo na desturi zilizozoeleka na kwa hekima yake:
Rejea:
1 Wakorinto 11: 2-12
2 Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.
3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.
9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.