Rais Samia ateuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Mabadiliko ya TabiaNchi

Rais Samia ateuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Mabadiliko ya TabiaNchi

Mama'ke Yesu ndiye alitusilimisha, sijamuona bila hijabu.

1 Wakorintho 11:6 BHN​

Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.

BHN: Biblia Habari Njema
Unaokoteza vifungu vichache vya biblia bila ya kuelewa mantiki na mazingira yake.

Hiyo ni barua ya Mtume Paulo kwa Wakorinto walioomba mwongozo toka kwa Paulo juu ya kufunika kichwa uiongiapo hekaluni.

Na Paulo aliwajibu kwa kadiri ya mapokeo na desturi zilizozoeleka na kwa hekima yake:

Rejea:

1 Wakorinto 11: 2-12

2 Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.

3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.
9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.
 
Unaibadili biblia kwa matamanio yako? Dah, pole sana, "kila mwanamke":

5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
Lakini pia ufahamu kuwa barua hiyo ya Paulo uliilenga jamii husika, na uhalisia wao.

Hao Wakorinto ilikuwa ni kama walivyo wahindi ambapo wanawake huwa na nywele ndefu kuliko wanaume, na nywele zao ilikuwa ni fahari yao kama wanawake mbele ya waume zao. Hivyo walishauriwa pale wajongeapo kwenye ibada, wafunike nywele zao zilizo ufahari kwa waume zao kwaajili ya utukufu wa Mungu. Maana yake wasioneshe ufahari wa waume zao wakiwa mbele za bwana.

Sasa, wewe na kipilipili, na kwa jamii ambayo nywele hazina ufahari wowote mbele ya mumeo, ufunike kipilipili kwa sababu ipi ilihali hata ukiwemo msikitini hakuna anayeharibu ibada yake kwa kuzitazama nywele zako kipilipili?

Lakini ukweli ni kuwa hakuna atakayehukumiwa kwa kufunika au kutofunika nywele. Unachotakiwa ni kuifunika roho yako ili isichangamane na uovu. Ndiyo maana Paulo anasema wazi kuwa kama Kanisa wala hilo la nywele na kufunika, haliwezi kulifarakanisha Kanisa.

13 Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?
14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?
15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.
16 Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
 
Back
Top Bottom