Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais Dkt. Samia Suluhu ametoa Shilingi milioni 10 kwa Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya ya Arusha ili kusaidia kukamilisha utaratibu wa kuanzisha Chama cha Ushirika cha waendesha bodaboda hao.
Aidha, Rais ametoa pikipiki mbili zitakazotumiwa na viongozi wa chama hicho kwa ngazi ya wilaya na mkoa ili kusimamia na kutatua changamoto za wanachama.
Fedha hizo zilikabidhiwa leo Jijini Arusha na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Ali Kawaida, wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Wilaya ya Arusha. Mkutano huo pia ulihusisha uzinduzi wa mfumo wa kidijitali wa utambuzi wa wanachama.
Kawaida, amebainisha kuwa waendesha bodaboda walikosa fedha za kukamilisha usajili wa ushirika huo, na msaada wa Rais utawasaidia kuimarisha shughuli zao.
Pia amewataka waendesha bodaboda kujisimamia kwa nidhamu, kuacha matumizi ya dawa za kulevya, na kutoshiriki kwenye uhalifu.
Soma, Pia: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025