Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia amesikitishwa na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo, Mkoani wa Dar es Salaam iliyotokea asubuhi ya leo Novemba 16.

Pia, Soma: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

"Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi.

Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii."

 
Ujenzi wa majengo makubwa kariakoo uangaliwe upya. Kwa sasa watu wengi wanajenga kienyeji, na watu wa mamlaka wakijifanya kufuatilia wanazibwa midomo kwa shilingi mbili tatu ujenzi wa hovyo unaendelea.
 
Ujenzi wa majengo makubwa kariakoo uangaliwe upya. Kwa sasa watu wengi wanajenga kienyeji na watu wa mamlaka wakijifanya kufuatilia wanazibwa midomo kwa shilingi mbili tatu ujenzi wa hovyo unaendelea.
Baada ghorofa changombe kuanguka...miaka michache nyuma.....kuna tume iliundwa kukagua majengo yote kariakoo na viunga vyake....cha ajabu hawakupata hata mmiliki mmoja kuwapa ushirikiano....
Zoezi lilikufa hapo ....sikuelewa kweli serikali imeshindwa kuwapata wamiliki kweli?
 
Kipindi hiki hajaagiza uchunguzi ufanyike?
 
Aliyemuandikia angeweka na sentensi hii: " ninawataka wataalam WA ujenzi kuanzia leo hii wafanye uhakiki WA haraka kuhusu ubora WA majengo yote yaliyopo jirani na eneo hili na jiji zima kwa ujumla.."
 
Ukiona kiongozi anatumia sana hizi kauli nasikitika, nashangaa, naumia, sio vizuri mnavyofanya, Mungu anawaona n.k ujue hapo hamna kitu
Hakuna kitu hapo, yaani ni kama na yeye pia kuna mtu mwingine anamsubilia ndo aje atoe suluhisho.

All in all, this is our Nation
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…