Rais Samia atoa pole ya Mil. 20, kwa Marehemu King Kikii na Fred Kisulwa.

cocochanel

Platinum Member
Joined
Oct 6, 2007
Posts
27,885
Reaction score
76,043
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa mkono wa pole kwa familia ya mwanamuziki mkongwe wa dansi, Marehemu Boniface Kikumbi "King Kiki" na familia ya Muigizaji marehemu Fred Kiluswa kwa kuwapatia rambirambi ya Shilingi Milioni 10 kila familia.

jamiiforums.jpg

Rambirambi hizo zimewasilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, alipotembelea familia hizo akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Taasisi ya mama Ongea na mwanao, Steve Nyerere, Asha Baraka, Muandaaji wa filamu William Mtitu na Ignus Mkindi leo Desemba 1, 2024 jijini Dar es Salaam.

Screenshot_20241202_052722_com_instagram_android_InstagramMainActivity_edit_138058296141760.jpg

"Kama tulivyoshirikiana kipindi cha kuuguza, Serikali imeona ni vyema kuendelea kuwashika mkono hata kipindi hiki cha majonzi, yaliyotokea ni mipango ya Mungu hatuna budi kuikubali lakini tunawaahidi kuwa tutaendelea kuwa pamoja" amesema Mhe Mwinjuma.
jamiiforums1.jpg

Marehemu King Kiki, ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 15, 2024, anakumbukwa kwa mchango wake katika muziki wa dansi, ambapo alitamba na nyimbo mbalimbali maarufu, ikiwemo "Kitambaa Cheupe."

cloudsfm.jpg

Vilevile marehemu Fred Kiluswa aliyefariki dunia Novemba 16, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mloganzila atakumbukwa kwa namna alivyokua anafanya vizuri katika filamu.

jamiiforums cloudsfm.jpg

Kutoka Clouds FM
 
Attachments

  • Screenshot_20241202_052921.jpg
    Screenshot_20241202_052921.jpg
    268.6 KB · Views: 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa mkono wa pole kwa familia ya mwanamuziki mkongwe wa dansi, Marehemu Boniface Kikumbi "King Kiki" na familia ya Muigizaji marehemu Fred Kiluswa kwa kuwapatia rambirambi ya Shilingi Milioni 10 kila familia.

View attachment 3167005

Rambirambi hizo zimewasilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, alipotembelea familia hizo akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Taasisi ya mama Ongea na mwanao, Steve Nyerere, Asha Baraka, Muandaaji wa filamu William Mtitu na Ignus Mkindi leo Desemba 1, 2024 jijini Dar es Salaam.

View attachment 3167009

"Kama tulivyoshirikiana kipindi cha kuuguza, Serikali imeona ni vyema kuendelea kuwashika mkono hata kipindi hiki cha majonzi, yaliyotokea ni mipango ya Mungu hatuna budi kuikubali lakini tunawaahidi kuwa tutaendelea kuwa pamoja" amesema Mhe Mwinjuma.
View attachment 3167008
Marehemu King Kiki, ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 15, 2024, anakumbukwa kwa mchango wake katika muziki wa dansi, ambapo alitamba na nyimbo mbalimbali maarufu, ikiwemo "Kitambaa Cheupe."

View attachment 3167007

Vilevile marehemu Fred Kiluswa aliyefariki dunia Novemba 16, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mloganzila atakumbukwa kwa namna alivyokua anafanya vizuri katika filamu.

View attachment 3167006

Kutoka Clouds FM
Umejitahidi leo kuandika bila kuchapia.Au umepata katibu muhtasi?
 
Serikali haiwezi kumaliza changamoto za wananchi wake kwa kugawa hela kwa mtu mmoja mmoja kama hivi.
Ni kampeni za urais tu hakuna lolote la maana,
Mara sijui goli la mama,mara sijui upuuzi gani!
Sasa kwa utaratibu huo watawafikia watu wangapi?
Kule mahospitalini kuna watoto wadogo wana magonjwa mazito sana na wazazi wao wanashindwa kumudu gharama za matibabu lakini hawawasaidii huku wanatapanya pesa ovyo tu.
Mtu ameshakufa unapeleka milioni 20 wafiwa wakagawane ndiyo nini sasa!
 
Back
Top Bottom