Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga; na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Mongoso Wambura, kufuatia vifo vya watu 32, wakiwemo Askari Polisi watatu, vilivyotokana na ajali mbili tofauti za barabarani, usiku wa kuamkia tarehe 09 Oktoba, 2026, mkoani Morogoro.
Rais Dkt. Samia anatoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, ndugu, jamaa na marafiki, na anawaombea nguvu, subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi. Aidha, anawatakia majeruhi wote uponyaji wa haraka.
Katika hatua nyingine, amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia sheria za usalama barabarani, na anawasihi madereva na watumiaji wote wa barabara kuchukua tahadhari na kuzingatia sheria ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.
Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema pseponi. Amin.
Soma Watu zaidi ya 30, wakiwemo Askari wa Jeshi la Polisi, wamefariki Dunia katika ajali Morogoro