PostGE2025 Rais Samia atumia vifungu vya Biblia na Qur'an kutoa wito wa toba

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais Samia Suluhu Hassan ametumia vifungu vya Biblia na Qur'an kutoa wito wa toba, unyenyekevu na kuomba msamaha kwa Mungu kufuatia Matukio ya Oktoba 29 yaliyoikumba nchi.

Akinukuu Biblia katika kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati 7:14, Rais Samia amesema, “Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”

Aidha, alinukuu pia Qur'an katika Surah Al-A'raf 7:23 inayosema, “Mola wetu! Tumejidhulumu nafsi zetu, na usipotusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara.”

Damu za watu zitamkalia kichwani jamani asifanye utani
 
Kwamba ni nini? Au cha ajabu ni kitu gani?

Hili nalo la kusifia,?

Kuna siku mtasema Rais kavaa viatu
 
Back
Top Bottom