Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Goba tunapata maji saa 8 usiku mara moja kwa wiki sijui wameona maji ganiHongera Mh. Rais
Anastahili, apewe maua yake na shukrani zake, ni October 29!. Japo Wengi Wamepania Kumzawadia Mwezi October 2025, Mimi Zawadi Yangu Nimemuaa Kuitoa Mapema, Kusubiria 2025 Will Be Too Little Too Late!Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Juu ya Heshima ya Maji (Presidential Global Water Changemakers Awards 2025) iliyotolewa na Global Water Partnerships kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika.
Tuzo hiyo imetolewa na Mheshimiwa Rais Duma Boko wa Jamhuri ya Botswana, ambaye ni Mwenyekiti wa "Presidential Global Water Changemakers Awards 2025" na kupokelewa kwa niaba yake na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana.
Tuzo hiyo iliyotolewa wakati wa Mkutano wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Barani Afrika, " AU - AIP Africa Water Investment Summit 2025", unaofanyika jijini Cape Town - Afrika Kusini kuanzia tarehe 13 -15 Agosti 2025, inatambua mchango mkubwa wa Mhe. Rais Samia katika uongozi na mageuzi kwenye Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji, usambazaji maji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na ubunifu wa kutafuta fedha za maji kupitia Hati Fungani ya Kijani (Green Bond) iliyotolewa na Mamlaka ya Maji Tanga.
Viongozi wengine waliotunukiwa tuzo hiyo kwa kutambua michango yao mbalimbali katika kuendeleza Sekta ya Maji kwenye nchi zao ni Mheshimiwa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini; Mheshimiwa Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal; Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE); Mwanamfalme (His Royal Highness Prince) Mohammed bin Salman Al Saudi, Mwanafalme (the Crown Prince) na Waziri Mkuu wa Falme ya Saudi Arabia na Mtukufu Mfalme Letsie III wa Falme ya Lesotho.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Jopo la Viongozi Mashuhuri katika Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji Barani Afrika (High Level Panel on Water Investments for Africa) anashiriki kwenye mkutano huo.
Washiriki takribani 600 kutoka nchi mbalimbali wanashiriki Mkutano huo akiwemo Mtukufu Mfalme Mswati wa III wa Falme ya Eswatini ambaye alishiriki sambasamba na Rais Boko katika utoaji wa tuzo hiyo.
Waafrica hupongezana kwa ujinga,just kwa sababu balozi zao maji yanatoka 24/7 wanadhani ndiyo maisha kumbe ni zaidi ya hivyo.Goba tunapata maji saa 8 usiku mara moja kwa wiki sijui wameona maji gani
Ungeshangaza ungeandika tofauti na ulichoandika hapa.Anastahili, apewe maua yake na shukrani zake, ni October 29!.
P
P
Tuzo zingine za mchongoTuzo nyingi sana anapata Mama,
Zimekua nyingi sanaTuzo zingine za mchongo
..mji mkuu dodoma unategemea maji ya kisima ya chumvi..huku mradi wa maji kutoka ziwa victoria ukiishia Tabora, licha ya kwamba ulipaswa sasa uwe umefika dodoma..Anastahili, apewe maua yake na shukrani zake, ni October 29!.
P
P
Wale masokwe Fulani watajinyea mwaka huu Kwa wivuRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Juu ya Heshima ya Maji (Presidential Global Water Changemakers Awards 2025) iliyotolewa na Global Water Partnerships kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika.
Tuzo hiyo imetolewa na Mheshimiwa Rais Duma Boko wa Jamhuri ya Botswana, ambaye ni Mwenyekiti wa "Presidential Global Water Changemakers Awards 2025" na kupokelewa kwa niaba yake na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana.
Tuzo hiyo iliyotolewa wakati wa Mkutano wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Barani Afrika, " AU - AIP Africa Water Investment Summit 2025", unaofanyika jijini Cape Town - Afrika Kusini kuanzia tarehe 13 -15 Agosti 2025, inatambua mchango mkubwa wa Mhe. Rais Samia katika uongozi na mageuzi kwenye Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji, usambazaji maji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na ubunifu wa kutafuta fedha za maji kupitia Hati Fungani ya Kijani (Green Bond) iliyotolewa na Mamlaka ya Maji Tanga.
Viongozi wengine waliotunukiwa tuzo hiyo kwa kutambua michango yao mbalimbali katika kuendeleza Sekta ya Maji kwenye nchi zao ni Mheshimiwa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini; Mheshimiwa Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal; Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE); Mwanamfalme (His Royal Highness Prince) Mohammed bin Salman Al Saudi, Mwanafalme (the Crown Prince) na Waziri Mkuu wa Falme ya Saudi Arabia na Mtukufu Mfalme Letsie III wa Falme ya Lesotho.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Jopo la Viongozi Mashuhuri katika Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji Barani Afrika (High Level Panel on Water Investments for Africa) anashiriki kwenye mkutano huo.
Washiriki takribani 600 kutoka nchi mbalimbali wanashiriki Mkutano huo akiwemo Mtukufu Mfalme Mswati wa III wa Falme ya Eswatini ambaye alishiriki sambasamba na Rais Boko katika utoaji wa tuzo hiyo.
anapendwa na kufanya vizuri mpaka nchi zingine wanakubali mkuu!!Tuzo nyingi sana anapata Mama,
ni KWELI DODOMA KUNA SHIDA KUBWA YA MAJI...SHIDA KUBWA SANA ...mji mkuu dodoma unategemea maji ya kisima ya chumvi..huku mradi wa maji kutoka ziwa victoria ukiishia Tabora, licha ya kwamba ulipaswa sasa uwe umefika dodoma..
Tuzo haiwez kubadilisha uhalisia..tuzo ya thamani ni ile unapewa na Mwenyezi Mungu, hizi zingine zote haziongezi chochote kwa mpokea tuzo!
Ukienda makabe msakuzi maramba mawili kwembe hakuna maji 😄Hivi mnatambua kwamba kuna watu katika hili taifa lenye maziwa yote makuu Afrika maji kwenye mabomba yanakatika kuliko upatikanaji wake ?!!!
In Abundance of Water a Fool is thirsty...., Hizi Tuzo wangewapa watu kule Jangwani mfano Libya au Egypt kutoa huku kwetu ni kama dhihaka....
Ngoja tusome komentis za haters tufurahi!Hongera Mh. Rais