Rais Samia atunukiwa Tuzo Maalam ya Maji (Presidential Water Changemakers Award 2025)

Rais Samia atunukiwa Tuzo Maalam ya Maji (Presidential Water Changemakers Award 2025)

2192C47C-C140-406E-9CC2-FCFE320F2CFB.jpeg
 
Haters punguzeni shobo ,mlitegemea SSH amalize shida zenu Kwa miaka 4 wakati mlikuwa na watu wanapiga domo tuu mkiwashangilia?

Mama apewe maua yake

View: https://www.instagram.com/reel/DM8UwJEIii0/?igsh=cGRhY2ZzMTZ0amR6

View: https://www.instagram.com/reel/DM-hIaeIyWD/?igsh=cnZuMWRvbWplMjVq

Unaongelea miaka minne wakati kila kitu kipo tayari ? Hii mifumo ilioyopo leo ni tangia Uhuru ila ndio hivyo matumizi yameongezeka kwahio shida zinatokea..., vyanzo vipo pale tu unaviona kwa macho nchi hii mvua sio tatizo ila ndio hivyo wakati zamani kulikuwa na mito isiyokauka sasa hivi mazingira wameharibu na mito imekauka ndio hao wengi ambao sasa hivi hata maji hawana (nchi yenye maziwa makuu yote Afrika) Alafu unasifia nini kama sio dalili za mediocrisy..., ila sishangai wakati tuna uwezo wa kuwa na umeme wa kumwaga bado watu / nchi wanahamasisha gesi wanayonunua kutoka ughaibuni (ili tu wachache waweze kunufaika)..., kwahio ndio haya haya muendelezo wa umimi / kutafuta ujiko kwa mgongo wa mwananchi kupata shida...

 
Unaongelea miaka minne wakati kila kitu kipo tayari ? Hii mifumo ilioyopo leo ni tangia Uhuru ila ndio hivyo matumizi yameongezeka kwahio shida zinatokea..., vyanzo vipo pale tu unaviona kwa macho nchi hii mvua sio tatizo ila ndio hivyo wakati zamani kulikuwa na mito isiyokauka sasa hivi mazingira wameharibu na mito imekauka ndio hao wengi ambao sasa hivi hata maji hawana (nchi yenye maziwa makuu yote Afrika) Alafu unasifia nini kama sio dalili za mediocrisy..., ila sishangai wakati tuna uwezo wa kuwa na umeme wa kumwaga bado watu / nchi wanahamasisha gesi wanayonunua kutoka ughaibuni (ili tu wachache waweze kunufaika)..., kwahio ndio haya haya muendelezo wa umimi / kutafuta ujiko kwa mgongo wa mwananchi kupata shida...

Umeandika pumba gani Sasa?
 
Umeandika pumba gani Sasa?
Kama huwezi kuelewa nilichoandika samahani kwa ku over estimate uelewa wako...; Unaongelea eti miaka minne umefanya mengi wakati hata hio miundombinu yote misingi yake ni tangia enzi za uhuru ? Tena bora kipindi hicho hata sewage system ilikuwa up to standard sasa hivi maji taka yanatupwa na mauchafu ziwani (no wonder magonjwa ya ajabu ajabu Kanda ya Ziwa yamejaa) Unaongelea upatikanaji wa maji safi sasa hivi kwa kuonyesha tenki wakati hapo walipoweka tanki huenda kabla wala kulikuwa hakuna uhitaji kwa kuwa nalo sababu kulikuwa na mito inayotiririka.... Sasa hivi tuna makusanyo ya kutosha tuna vyanzo vya kutosha kuliko nchi yoyote Afrika na bado majority hawana maji (and now it is worse sababu kuna mito imekauka)

Na bado tukiwa katika category hio hio, ya mazingira bado tunaonyesha ukosefu wa busara kwa kutumia kodi zetu kwa kununua gesi kutoka ughaibuni (Au huoni connection ya Nishati na Kukauka kwa Mito na Disposable Income ya Mbangaizaji)?
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Rais ya Kimataifa ya Wabunifu wa Mabadiliko katika Sekta ya Maji 2025 (Presidential Global Water Changemakers Award 2025), heshima kubwa inayotolewa na taasisi ya maji duniani, ( Global Water Partnership) kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika.

Tuzo hiyo imetolewa rasmi na Rais Duma Boko wa Jamhuri ya Botswana, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tuzo za Rais za Kimataifa za Wabunifu wa Mabadiliko katika Sekta ya Maji 2025, ambapo kwa niaba ya Rais Samia, tuzo ilipokelewa na Balozi James Bwana, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Tuzo imetolewa wakati wa Mkutano wa Kilele wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji wa AU-AIP 2025, ulioanza jijini Cape Town, Afrika Kusini, na unatarajiwa kumalizika tarehe 15 Agosti 2025.

Global Water Partnership imetambua uongozi bora na jitihada za mageuzi za Rais Samia katika sekta ya maji, ikiwemo uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya maji, upanuzi wa huduma ya maji safi kote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mikakati bunifu ya ufadhili kama vile hati fungani ya Kijani (Green Bond) lililotolewa na Mamlaka ya Maji ya Tanga chini ya Wizara ya Maji.

Chanzo: Nipashe
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Juu ya Heshima ya Maji (Presidential Global Water Changemakers Awards 2025) iliyotolewa na Global Water Partnerships kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika.

Tuzo hiyo imetolewa na Mheshimiwa Rais Duma Boko wa Jamhuri ya Botswana, ambaye ni Mwenyekiti wa "Presidential Global Water Changemakers Awards 2025" na kupokelewa kwa niaba yake na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana.
Tuzo hiyo iliyotolewa wakati wa Mkutano wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Barani Afrika, " AU - AIP Africa Water Investment Summit 2025", unaofanyika jijini Cape Town - Afrika Kusini kuanzia tarehe 13 -15 Agosti 2025, inatambua mchango mkubwa wa Mhe. Rais Samia katika uongozi na mageuzi kwenye Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji, usambazaji maji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na ubunifu wa kutafuta fedha za maji kupitia Hati Fungani ya Kijani (Green Bond) iliyotolewa na Mamlaka ya Maji Tanga.

Viongozi wengine waliotunukiwa tuzo hiyo kwa kutambua michango yao mbalimbali katika kuendeleza Sekta ya Maji kwenye nchi zao ni Mheshimiwa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini; Mheshimiwa Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal; Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE); Mwanamfalme (His Royal Highness Prince) Mohammed bin Salman Al Saudi, Mwanafalme (the Crown Prince) na Waziri Mkuu wa Falme ya Saudi Arabia na Mtukufu Mfalme Letsie III wa Falme ya Lesotho.

Mheshimiwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Jopo la Viongozi Mashuhuri katika Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji Barani Afrika (High Level Panel on Water Investments for Africa) anashiriki kwenye mkutano huo.

Washiriki takribani 600 kutoka nchi mbalimbali wanashiriki Mkutano huo akiwemo Mtukufu Mfalme Mswati wa III wa Falme ya Eswatini ambaye alishiriki sambasamba na Rais Boko katika utoaji wa tuzo hiyo.
Atatunukiwa nishani nyingi sana. Bado nyingine zinaandaliwa:

1. Nishani ya Rais wa kwanza mwanamke kuwa dikteta katika bara la Afrika.

2. Nishani ya kuwa Rais wa kwanza kuuza rasilimali za Tanganyika kwa waarabu, na kuwateka wanaomkosoa na kumkemea kupora rasilimali za Taifa.

3. Nishani ya kuwa Rais wa kwanza kumfunga mpinzani wake ili asipate ushindani wakati wa uchaguzi

4. Nishani ya kuwa Rais wa kwanza kuteka na kuua wakosoaji wake wengi kuliko kiongozi mwingine yeyote wa Tanzania.

Huyu atapokea nishani nyingi sana, maana aliyoyafanya, mengi hayajawahi kufanywa na yeyote. Msimdhulumu hizo ni nishani zake.
 
Back
Top Bottom