Rais Samia atunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, leo Aprili 18, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, leo Aprili 18, 2024 kutambua Jitihada zake za Kuendeleza Mageuzi ya Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi-4R.


View: https://youtu.be/k_A0yON0ZXg?feature=shared


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wageni, viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Kikuu Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo.
PIA SOMA:
- Mama Samia Atunukiwa Udaktari wa Uchumi (Doctorate of Economics Degree) Uturuki

- Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi ya Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), leo Desemba 28, 2023

- Rais Samia ashiriki Mahafali ya 52 Duru ya 5 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Atunukiwa Shahada ya Heshima

- Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru chamtunuku Rais Samia Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), leo Oktoba 10, 2023

- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Anga cha Korea (KAU) leo tarehe 03 Juni, 2024.
 
Ni jambo jema 😄

Yesu alisema " mama Tazama mwanao, Mwana Tazama mama yako"

Hiyo ndio Uturuki 😄😄🌹
 
Sasa hiyo doctorate magumashi inatusaidia nn sie wananchi wa huku Namtumbo??.
Nadhani ile halisi ndo inaweza kuwa na kitu kichwani kusudi ilete matunda ktk field.
 
Mkuu Roving Journalist , asante sana kwa taarifa hii, jf is doing a very good job ya uhabarishaji.
P
 
Ni jambo jema aje autumie kwa vitendo kwa kina Mwigulu
 
Hivi matukio na matatizo na ajari zinazotokea hapa bongo kweli kiongozi anapata mda wa kwenda kupokea udaktali wa ofa R.I.P JPM japo ulikua na majibu magumu kwa wahanga lakini ulikua unaenda kuwaona na kuwaambia wakomae hakuna cha bure
 


Mama bado sana hata tume huru imemshinda bado katiba. Wangempa PHD ya utalii ndiyo amefanya vizuri mpaka sasa.
 
Napendekeza kuheshimu heshima kubwa aliyoipatia TZ, aanze kutambulishwa rasmi kwa degree zote mbili, yaani Mh. Daktari, Daktari ......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…